Header Ads

BUTABILE AUNGURUMA KWA WANANCHI, AAPA KUTATUA KERO KWA ASILIMIA 100

DIWANI wa Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro, Mhe. Thomas Butabile amekutana na wananchi wa Mtaa wa Madox Msufini ikiwa ni ziara yake ya Mtaa kwa Mtaa  kwa ajili ya kusikiliza kero ambazo wanakabiliana nazo ,kusema utekelezaji wa Ilani pamoja na kupokea ushauri ikiwa ni ziara yake ya Mtaa kwa Mtaa awamu ya pili.

Katika ziara hizo zilizoanza Novemba 01/2023, Mhe. Butabile, aliambatana timu ya Wataalamu mbalimbali kutoka Ofisi ya Kata na Ofisi nyengine za Umma.

Mhe. Butabile, amesema kuwa huo umekuwa ni utaratibu wake aliojiwekea kwanza kukagau miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi ili kutoa fursa kwa Wananchi kubainisha changamoto zao na yeye kwenda kuzitatua na nyengine kuzibeba kuzifikisha ngazi za Juu kwa ajili ya utatuzi.

Akizungumza na Wananchi wa Mtaa wa Madox, Mhe, Butabile, amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kutoa fedha ili kutekekeleza miradi kwenye Sekta ya Elimu, Maji, Afya , miundombinu ya maji , Umeme na barabara kama Ilani ya CCM inavyoelekeza.

Pia Butabile, amesema tangia aingie madarakani mwaka 2020, Viwango vya  ufaulu katika kata yake vimeimarika kuanzia shule za Msingi na Sekondari.

Lakini pia amekuwa na mchango mkubwa hususani katika kuhamasisha wananchi ujenzi wa madarasa jambo ambalo alifanikiwa kwa kiasi kikubwa .

"Mimi  nimeanza ziara yangu ya Mtaa kwa Mtaa kusikiliza kero nikiwa na Wataalamu wangu, niombe Viongozi wa Serikali za Mitaa na Watendaji wenu mfanye  mikutano na wanchi mara kwa mara ili kusikiliza kero zao na kuzifanyia kazi, tusingoje mpaka Viongozi wajuu waje ndio wananchi wanyooshe mabango, tutimize wajibu wetu kama kero unaona ipo nje ya uwezo wako usikae nayo peleka ngazi za juu ili ipatiwe ufumbuzi na kutaturiwa , tusirundike kero za wananchi Ofisini " Amesema Mhe. Butabile.

Kuhusu Vitambulisho vya NIDA , Mh. Butabile,  amewataka wananchi ambao hawajafanikiwa kupata namba za Utambuzi wa Vitambulisho vyao wafuate taratibu ili waweze kupatiwa namba hizo  huku akihimiza wataalamu kuendelea kutoa elimu ya namna ya kupata  namba za utambuzi pamoja na Vitambulisho.

Ziara hiyo ya Mtaa kwa Mtaa inaendelea leo Novemba 02/2023 katika Mtaa wa Kidongolo A.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.