Header Ads

MANISPAA ILEMELA YAFURAHISHWA NA USIMAMIZI BORA WA STENDI YA MABASI MSAMVU



HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela Mkoa wa Mwanza, ikiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Mhe.Renatus Mulunga,  imeridhishwa na namna Manispaa ya Morogoro  imekuwa ikisimamia mifumo ya ukusanyaji  mapato na usimamizi mzuri wa Stendi ya Mabasi Msamvu pamoja na uendeshaji wa Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro .

Pongezi hizo zimetolewa Novemba 20/2023 katika ziara ya Manispaa ya Ilemela ya kujifunza uendeshaji wa Stendi ya Mabasi Msamvu.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara , Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Mh.Renatus Mulunga, amesema  kuwa  wameshuhudia ubora wa hali ya juu katika majengo yote waliyotembelea na kuwa wameridhishwa na namna Manispaa ya Morogoro inavyomsaidia  Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

"Wenzetu mna miradi mizuri wa kimkakati na sisi tunakwenda kuwa na stendi ya kisasa, lengo la ziara ni kujifunza uendeshaji wa Stendi , tumeona vitu vizuri na sisi tukifika Ilemela tutajipanga na wataalamu wangu kuhakikisha yale ambayo tumejifunza tunakwenda kuyafanyia kazi  nina imani na timu yangu na Baraza langu la Madiwani  " Amesema Mh. Mulunga.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro,Mhe. Pascal Kihanga,  ameshukuru Manispaa ya Ilemela kufanya ziara Manispaa ya Morogoro kwani Manispaa ya Morogoro imekuwa chuo cha kujifunzia miradi ya Kimkakati.

Miongoni mwa miradi ambayo Manispaa ya Ilemela imetembelea Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kujifunza ni pamoja na Soko Kuu la Chifu Kingalu pamoja na Stendi ya Mabasi Msamvu.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.