JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA MOROGORO MJINI YAKABIDHI VITENDEA KAZI KWA VIONGOZI WA KATA JUMUIYA
JUMUIYA ya Wazazi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, imekabidhi vitendea kazi kwa Viongozi wa kata ili kurahisisha utendaji kazi.
Vitendea kazi hivyo vimegaiwa Novemba 15/2023 kwenye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kata ya Kingo ambapo Kaimu Katibu wa Jumuiya hiyo akiwa na wajumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Wilaya waliendesha zoezi hilo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vitendea kazi hivyo ikiwemo Limu paper na Kata na Kanuni kwa kila Kata kwa kata 29, Kaimu Katibu Wazazi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya, Sabrina Juma, amesema lengo la vitendea kazi hivyo ni kurahisisha utendaji kazi kwa Viongozi katika kutimiza majukumu yao.
"Tumegawa vitendea kazi japo kwa uchache lakini naamini kazi zitafanyika, naomba mtuamini viongozi wenu tunapambana kwa ajili yenu, Kamati yenu ya Utekelezaji ipo makini sana, kama kuna changamoto mahali namba yangi ipo wazi mnataka maelekezo au majibu ya jambo nipigieni nitatoa ufafanuzi, kanuni mkazisome vizuri ili Jumuiya yetu iwe ya mfano " Amesema Sabrina.
Aidha, Sabrina amewataka Viongozi kujitahidi kuongeza idadi ya wanachama wa Jumuiya huku akitoa rai kuwa Viongozi wanaomba kadi za jumuiya wachukue na za Chama kwani ndio utaratibu ambao upo ili kuwa namba sawa kati ya Chama na Jumuiya.
Pia, amesema atatoa muongozo kwa Viongozi wa Kata juu ya semina ambayo itasimamiwa na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Wilaya ambapo wajumbe hao wataanza kwenye Kata zao wanapoishi na baada ya hapo watahamia kwenye Kata nyengine lengo ni kuimarisha uhai wa Jumuiya.
Post a Comment