HALMASHAURI KUU CCM WILAYA YA MOROGORO MJINI YAFURAHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM MANISPAA YA MOROGORO.
MKUTANO wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Morogoro Mjini imefurahishwa na utakelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Manispaa ya Morogoro .
Pongezi hizo zimetolewa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Morogoro Mjini , Novemba 16/2023 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa DDC Mbaraka Mwishehe Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na wajumbe katika kikao hicho, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Fikiri Juma,amesema ameridhishwa na utekelezaji wa Ilani kufuatia ziara yake ya Kamati ya siasa aliyoifanya Mwezi Oktoba ya kukagua miradi ya maendeleo.
Fikiri,amelipongeza Baraza la Madiwani kwa kushirikiana na Menejimenti ya Manispaa kwa usimamizi mzuri na wa uwazi katika kusimamia miradi ya Maendeleo.
Aidha, Fikiri, ametoa pongezi kubwa kwa Madiwani wote wa Manispaa ya Morogoro , Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Wabunge wa Viti Maalum kwa kazi kubwa wanazozifanya za kuwaletea wananchi maendeleo.
“zipo changamoto lazima zifanyiwe kazi na maelekezo nimetoa kwa Manispaa na Taasisi za Umma , lakini kasi hii ya utekelezaji wa Ilani hapa Morogoro Mjini , hatuna cha kumlipa Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan zaidi ya kumuahidi ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika 2024 na uchaguzi Mkuu mwaka 2025 ”Amesema Fikiri.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Hilary Sagara, amesema Ofisi ya Mkuu wa Wilaya itaendelea kusimamia miradi pamoja na kupokea maelekezo yote ya CCM kwa ajili ya utekelezaji wa Ilani ikiwemo kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro , Mhe. Pascal Kihanga, amesema , Manispaa ya Morogoro imejipanga kimkakati kwani ile ndoto ya kuwa Jiji inakwenda kutimia kutokana na kusogelea kukidhi vigezo vya kuwa Jiji.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, MD Machela, amesema Manispaa imekamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya Shule, huduma ya afya , huduma ya masoko kwa kuwa na masoko mazuri yenye hadhi kwa wafanyabiashara kama vile Mabanda ya wamachinga .
“watumishi wapo tayati kutekeleza Ilani hasa kwa kipindi hiki kabla ya uchaguzi, tunashukuru CCM kupitia Kamati yako ya Siasa na Halmashauri Kuu kwa kuendelea kutusimamia na kutukosoa pale tunapokosea katika utendaji wetu wa kazi” Amesema Machela,
Machela ,amesema kero kubwa ilikuwa ni miundombinu ya barabara ambapo kupitia miradi ya Tactics Manispaa ilikuwa na kilomita 10 lakini mpaka sasa wamepambana wamepata kilomita 20.5 kwa jili ya utengenezaji wa barabara kwa viwango vya lami .Pamoja na miradi ya barabara ,
MD Machela,amesema kuwa kuna ujenzi wa mifereji yenye kilomita 4.4 itakayojengwa kwa zege ili kupunguza mafuriko katikati ya Mji
Post a Comment