Header Ads

WANANCHI WA KATA YA MAFIGA WATAKA NIDA KUWALETEA VITAMBULISHO KWENYE KATA YAO.

BAADHI  ya wananchi wa kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro wamezitaka ofisi za NIDA kuwaletea vitambulisho vyao kwenye kata yao.

Wamezungumza hayo Novemba 14/2023 katika  ziara ya Diwani wa kata ya hiyo Mh Thomas Butabile wakati akisikiliza na kutatua kero za wananchi mtaa wa Ngazengwa.

Wananchi wamefafanua kuwa Ofisi za NIDA zimekuwa ni changamoto hawatoi huduma kwa wakati na vitambulisho mpaka wavifuate Tungi wakati walikuja kuwaandikisha kwenye kata yao ambapo inapelekea wanatumia gharama kubwa ya nauli na wakifika hawahudumiwi.

Naye Diwani wa Kata hiyo, Mh Butabile amekili kuwepo kwa changamoto hiyo na kufafanua kwamba tayari ameisha ziagiza ofisi za Nida kuwapatia vitambulisho kwenye kata zao na wananchi kupatiwa kutoka kwa wenyeviti wa serikali za mtaa.

Sambamba na hayo Butabile amewataka wananchi kuwawavumilivu kwa sababu NIDA  tayari taarifa wanayo na wanasubiri Utekelezaji.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.