Header Ads

WAJANE WATAKIWA KUTOKUKATA TAMAA

DIWANI wa Kata ya Lukobe, Mhe. Selestin Mbilinyi, amewataka wajane  kutokata tamaa licha ya kupitia changamoto mbalimbali katika kutunza na kulea familia zao kutokana na kuondokewa na wapendwa wao.

Hayo ameayzungumza katika Uzinduzi wa Chama Cha Wajane Kata ya Lukobe, Novemba 25/ 2023.

Mhe. Mbilinyi, amesema anatambua kuwa wajane wakakumbana na changamoto nyingi lakini ni muhimu kutokata tamaa na kuhakikisha wanjishughulisha na ujasiriamali ili kuweza kumudu kulea familia zao.

Amesema kuwa  kutokana na kundi hilo kukabiliwa na changamoto nyingi anaiomba Serikali kulipatia msaada utakaowawezesha kujikwamua na kubadilisha maisha yao kwa kuwaingia katika makundi yanayopaswa kupata mikopo ya halmashauri.

“Tunaiomba Serikali ili kundi la wajane lijitegemee katika upewaji wa mikopo , lakini pia wasikate tamaa kwani kuondokewa na wenza wao ni njia ambayo kila mtu ataipitia kikubwa watazame maisha ya mbele kwa kujishughulisha na ujasiriamali ili walee familia zao" Amesema Mhe. Mbilinyi.

Aidha, Mbilinyi, amesema  wakati sasa Serikali inapaswa kuweka mpango utakaohakikisha kila mtaa kundi hili linafunguliwa mradi wa pamoja ili waweze kuondokana na unyonge na hatimaye waweze kuzisaidia familia zao.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wajane Mkoa wa Morogoro, Bi. Doroth Mwamsiku, amesema ujane sio mwisho wa maisha hivyo amewataka Wajane wapambane kuhakikisha familia zao zinaendelea kustawi.

Mwamsiku pia,ameiomba Serikali iwatazame kwa jicho pana wajane ili kuwasaidia kufikia malengo na kujiona kuwa hakuna walichokipoteza wapo sawa na wale ambao wana wenza wao.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.