KISHINDO CHA MIAKA 3 YA DIWANI KATA MAZIMBU UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO
MIAKA 3 sasa tangu Diwani wa Kata ya Mazzimbu, Mhe. Pascal Kihanga, kuapishwa na kuingia madarakani baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Mara baada ya Kuapishwa, Mhe. Kihanga kwa kuashirikiana na BMK ya Kata , alianza kutekeleza na kusimamia miradi mbalimbali ya Kata kwa kushirikiana na Wananchi wake pamoja na kuongozwa na Chama chake kilichompa Dola Chama Cha Mapinduzi CCM .
Kwa kipindi cha Miaka 3, Mhe.Kihanga , ameendelea na utekelezaji wa shughuli za Serikali na usimamiaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo katika miaka 3 aliyopo madarakani zipo fedha mbalimbali zimetumika kwenye miradi ikiwemo fedha zake binafsi, fedha za Wananchi , wadau , fedha kutoka Serikali Kuu na fedha kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.SEKTA YA ELIMU MSINGI
Katika Idara ya ya Elimu Msingi, tangia aingie madarakani kwa kushirikiana na BMK , tayari ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa shule ya Msingi Mazimbu A ambapo Manispaa ya Morogoro imeingiza milioni 15,000,000/= pamoja na chumba 1 na matundu 3 ya vyoo kupitia mradi wa Boost uliogharimu milioni 27,400,000/=.
Kwa upande wa Shule ya Msingi Mazimbu B , amekamilisha ujenzi wa wa chumba 1 cha darasa milioni 15,000,000/= zimetumika fedha kutoka Manispaa ya Morogoro.
Upande wa Sekondari Mazimbu, tayari milioni 100 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Utawala fedha kutoka Manispaa ya Morogoro.
Hali ya ufaulu.
Mazimbu ina shule 2 za Msingi Mazimbu A wanafunzi 1,722 na Mazimbu B 1,429 na Mazimbu Sekondari wanafunzi 913.
Matokeo ya darasa la saba 2023, Mazimbu A waliofanya mtihani ni 195 sawa na wastani wa 214.9282 na wote wamefaulu na Mazimbu B waliofanya ni 182 na waliofaulu 173 sawa na wastani wa 191.1429.
Kwa matokeo hayo Shule ya Mazimbu A imeongoza kwa vipindi 8 mfululizo na kuwa shule ya kwanza kwa upande wa Shule za Serikali Manispaa ya Morogoro.
SEKTA YA AFYA
Katika Sekta ya Afya, kwa kipindi cha Miaka 3 ya Utawala wa Mhe. Kihanga, Kata ya Mazimbu kwa sasa ipo katika hatua ya mwisho kukamilisha mradi wa Kituo cha afya.
Katika ujenzi huo, Mhe. Kihanga,amesema jumla ya milioni 135,000,000/=zimeshatumika kuhakikisha mradi huo unakamilika ili kutoa huduma za kiafya na kuwasogezea wananchi huduma karibu na kuacha kufuata huduma umbali mrefu kwenda katika vituo vyengine vya afya.
Idara ya Maendeleo ya Jamii
Kata ya Mazimbu kupitia Ofisi ya Afisa Mtendaji kwa kushirikiana na Afisa Maendeleo ya Jamii na Afisa Ustawi zipo shughuli ambazo zimefanyika ikiwemo kufuatilia madeni ya vikundi vilivyokopeshwa mkopo wa asilimia 10 Manispaa , kutoa elimu ya ukatili wa jinsia na namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa waendesha bodaboda, ambapo vijiwe 2 vimefikiwa na elimu hiyo ikiwemo vijana 14 walifikiwa na elimu huku zoezi hilo likiwa ni endelevu kwa vijiwe vyote ndani ya Kata.
Utoaji wa elimu ya ukatili shuleni jumla ya wanafunzi 1,382 walifikiwa na elimu kati yao 687 wanaume na 695 wasichana kutoka shule ya Msingi Mazimbu B na zoezi hilo linaendelea kwa shule zote ndani ya Kata kwa kushirikiana na CDO, PSW, pamoja na Polisi Kata.
Aidha, Ofisi ya Kata imeendelea kusikiliza mashauri mbalimbali ikiwemo ndoa 1 , utoro 2 na mapenzi ya jinsia moja 1,na madai 2 ambapo shauri la mapenzi ya jinsia 1 limepewa rufaa kwenda Paralegal na mashauri mengine yamefanyiwa kazi na kumalizika na Ofisi inaendelea kusikiliza mashauri kwa kushirikiana na CDO, Watendaji wa Mitaa, PSW.
MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MIFEREJI
katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara , Mhe. Kihanga,amesema kulikuwa na barabra korofi ya barakuda lakini barabara hiyo imetengenezwa kwa kiwango cha lami na sasa kuna mpango wa kujenga mfereji wa maji barabra ya barakuda kupitia mradi wa tactics.
Mhe. Kihanga, amesema Manispaa ya Morogoro imetenga Milioni 700 mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajiili ya kununua greda ambalo litatumika kuboresha barabara za ndani ya Manispaa ya Morogoro .
SEKTA YA KILIMO
Kata ya Mazimbu ina jumla ya wakulima wa ndani 151 na wakulima wa nje 296 ambapo eneo la kilimo linalohudumia wakulima wa ndani ni hekari 14 na idadi ya kaya zinazoshiriki shughuli za kilimo ndani ya Kata na nje ni 4,046.
Mhe. Kihanga, amesema wakulima waliopatiwa mbolea ya ruzuku wamefanikiwa kuzipata kulingana na uwezo wake, ukubwa wa eneo na zao wanalolima ambapo Kata ya Mazimbu imefanikiwa kuwa na shamba la mfano la mahindi Mtaa wa Reli na liemfanya vizuri.
Katika upande wa idara ya mifugo, Mhe. Kihanga amesema Mazimbu imejikita katika kuhakikisha kuwa mifugo na uvuvi vinazalishwa kwa tija kwa kuinua kipato cha Kaya na uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Mhe. Kihanga, amesema Kata ya Mazimbu inaendelea na huduma mbalimbali za tiba za mifugo, ukaguzi wa wanyama , usafi wa machinjio na bucha za kuuzia nyama , udhibiti wa taka ngumu pamoja na ukaguzi wa Taasisi.
HUDUMA YA MAJI
Mhe. Kihanga ,amesema Kata hiyo haina changamoto kubwa sana ya Maji lakini maeneo ambayo kuna changamoto ya maji tayari taarifa ameshazifikisha kwa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Morogoro (MORUWASA ).
ANWANI ZA MAKAZI
Kata ya Mazimbu , ni miongoni mwa Kata 29 ambazo zimenufaika na utekelezaji wa mradi wa Anwani za Makazi ambapo hadi hivi sasa Utekelezaji huo umefikia asilimia 100 ambapo mradi huo utasaidia Kila Mkazi wa Kata hiyo kutambuliwa na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwani zoezi hilo lilihusisha uwekaji wa Namba za Nyumba, Majina ya Mtaa na Postikodi ambapo faida kubwa ya anwani za makazi ni kutusaidia kukuza na kuboreshwa kwa huduma za Ulinzi na Usalama ndani ya Jamii, kufanyika na kukuza kwa biashara Mtandaoni kidigitali na Kusaidia Serikali kufikisha huduma kwa wananchi kirahisi kulingana na Mahitaji ya eneo husika.
Mwisho, Mhe. Kihanga, amesema katika kipindi cha mika 2 iliyobakia ataendelea na Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Kimaendeleo ili kukuza Uchumi wa Kata ya Mazimbu , Kuzalisha ajira na kuongeza Ustawi wa Maisha ya Wananchi wa Mwembesongo katika kipindi chote cha Utawala wake.
Kwa upande wa Afisa Tarafa Manispaa ya Morogoro, Winfred Kipako, amewataka wananchi kuwaamini viongozi wao kwani yote wanayoyafanya ni kwa ajili ya maendeleo yao.
Kipako, amesema Manispaa ya Morogoro imetulia yote ni kwa jili ya Mstahiki meya kwa kushirikiana na Baraza lake la Madiwani walivyo na masikilizano na kuifanya Manispaa kuwa na maendeleo makubwa na kusogelea kuwa Jiji.
Post a Comment