MBUNGE ABOOD AKABIDHI VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA MILIONI 10.3 KWA ZAHANATI 5 MANISPAA YA MOROGORO
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaaziz Abood, amekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 10.3 kwa Zahanati 5 Manispaa ya Morogoro kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo.
Ugawaji wa Vifaa Tiba umefanyika Oktoba 30-31/2023 kwenye Zahanati 4 na Kituo cha Afya 1 ikiwemo Zahanati ya Sultan Area, Zahanati ya Kiwanja cha Ndege, Zahanati ya Mbuyuni, Zahanati ya Kihonda Maghorofani na Kituo cha Afya Sina Kata ya Mafisa.
Miongoni mwa Vifaa Tiba vilivyotolewa katika Zahanati hizo, ni Darubini 5 (Microscope), Kifaa cha kutenganisha selamu na seli za damu ( Centrifuge Mashine 5), Kifaa cha kupimia sukari ( Glucopus ) 5, Kitanda cha kumuangalia mgonjwa (Examination bed 2) pamoja na Jiko Dogo la Gesi 1.
Mhe. Abood, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wanawake wa Jimbo la Morogoro Mjini, wanajifungua kwenye mazingira salama.
Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe Manispaa ya Morogoro, Dkt. Maneno Matawa, amewashukuru Mbunge Abood, kwa Mchango wake hususani kwenye sekta ya afya huku akieleza kuwa Vifaa vyote tiba ambavyo wamevipokea vitakwenda kufanya kazi kama ilivyokusudiwa pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kukidhi mahitaji ya wananchi.
Naye Katibu wa Mfuko wa Jimbo la Morogoro Mjini, Elizabeth Badi, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro amesema kuwa Manispaa itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali pamoja na Ofisi ya Mbunge katika kuboresha naisha ya wananchi kwa kutoa elimu za kuelimisha jamii kuhusu afya kwa kutumia vikundi mbalimbali vya sauti za umma, kuwapa semina wataam wa afya na kutoa vifaa kwaajili ya Zahanati zote.
Post a Comment