Header Ads

WANUFAIKA WA TASAF MANISPAA YA MOROGORO WATAKIWA KUTOBWETEKA NA MAFANIKIO WALIYOYAPATA.



Mlengwa wa Mfuko wa maendeleo ya Jamii-TASAF akikabidhiwa fedha .
Mratibu wa TASAF Manispaa ya Morogoro, Feliciana Katemana akiongea na walengwa wa mfuko huo.

MRATIBU  wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF Halamshauri ya Manispaa ya Morogoro, Feliciana Katemana,  amewataka Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia TASAF kutumia fursa hiyo kwa ukamilifu kwa kufanya kazi kwa bidii  ili  kutimiza azma ya serikali ya kupambana na umaskini nchini.

Zoezi la kupitia majina ya walengwa wa TASAF. 
Hayo ameyasema leo Januari 16. 2020 wakati akikagua na kujionea utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika Kata ya Mwembesongo. 

Amesema  Serikali ya Awamu ya Tano inafanya juhudi kubwa za kuweka mazingira mazuri kwa  Wananchi kujiletea maendeleo na kuboresha maisha yao hivyo akawataka kutumia vizuri fursa hiyo kwa kufanya kazi za uzalishaji mali kwa bidi ili kukuza uchumi wao na hatimaye kuchangia katika pato la taifa na kuondoa kero ya umaskini miongoni mwao kwa vitendo.







Amesema kuwa Manispaa ya Morogoro katika mradi wa TASAF wamepokea jumla ya Shilingi Milioni 119 kwa kipindi cha Mwezi Machi na Aprili mwaka jana 2019 huku akiwataka Wananchi kuwa na subira kwani Serikali yao ni tulivu na itawapatia watu wote walionasifa katika mradi huo bila ubaguzi wa aina yoyote.

Hata hivyo amesema kuwa , fedha hizo zimegaiwa kwa walengwa wapatao 2945 katika kata zote 29 za Manispaa ya Morogoro ikiwamo Mitaa 164.

Katemana amewataka Walengwa wa TASAF kutobweteka na mafanikio waliyoanza kuyapata kutokana na huduma zinazotolewa na Serikali kupitia TASAF badala yake waendelee kuuchukia umaskini kwa vitendo kwa kufanya kazi kwa bidi ili  hatimaye waweze kuboresha maisha yao huku akisisitiza ustawi wa jamii kwa ujumla hususani watoto kama ilivyo dhamira ya Serikali.

Katika hatua nyingine , Katemana , ameuagiza Uongozi na Watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF katika ngazi za Kata kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu mkubwa na kuzingatia  Uzalendo kwani amesema Mfuko huo unagusa nyanja muhimu za Maendeleo ya Wananchi katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, afya,maji,uchumi,kilimo,mifugo na hifadhi ya mazingira na hivyo kuwa miongoni mwa sekta zinazogusa maisha ya wananchi wengi moja kwa moja.

“Serikali inathamini mchango wa taasisi hii katika jitihada zake za kupunguza umaskini nchini, endeleeni kufanya kazi kwa bidi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa haraka na ufanisi mkubwa” amesisitiza Katemana.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogor, Sheilla Lukuba, amesema kumekuwa na mafanikio makubwa katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo yaliyochangiwa kwa kiwango kikubwa na Serikali,Wadau wa Maendeleo na Wananchi hususani Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao amesema kwa sehemu kubwa wameanza kuboresha maisha yao na kuonyesha namna wanavyouchukia umaskini kwa vitendo.

Kwa upande wake, mnufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini ,  Bunga Mogela, ameishukuru Seriklai ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais Magufuli huku akikiri kuwa  mpango huo umekuwa mkombozi mkubwa kwao kwani umeweza kuwabadilisha kimaisha na kuiomba serikali kuongeza kiwango cha ruzuku ili kilingane na thamani halisi ya fedha kwa sasa.

Naye Antari Shadadi,  mkazi wa kata ya Mwembesongo, amesema kuwa kwa sasa anajishughulisha na ununuzi wa Mkaa pamoja na kusomesha Watoto kupitia biashara hiyo huku akimuomba Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kuendelea na moyo huo huo wa kuwasaidia walala hoi na watu wenyevipato vya chini katika Kaya Masikini.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.