Header Ads

Uongozi wa Dampo la takataka Manispaa ya Morogoro wakalia kuti kavu.


Mkurugenzi akikagua Dampo, kushoto afisa Mazingira Manispaa, Samwel Subi.
Eneo la Dampo ambalo lipo wazi takataka hazifiki katika eneo hilo takribani nusu ya dampo halina takataka.





Akizungumza na Waandishi wa Habari , amesema hajaridhishwa na Uongozi wa Dampo hilo kutokana na uharibifu unaoendelea kufanywa na Viongozi husasni katika suala zima la uchimbaji wa Vifusi vya mchanga na kuvipeleka sehemu isiyojulikana.
Mitambo ya magari taka kama yanavyoonekana hapo yakiwa katika matengenezo.
Aidha, amesema katika kikao cha kusikiliza na kutatua kero za Wananchi mnamo januari 8, 2020 kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi, St. Monica Kihonda, kuliibuka kero za kwamba kuna zoezi la uchimbaji wa  Vifusi unaoendelea katika Dampo hilo.

"Nipo hapa Dampo, ni  kweli nimejionea mwenyewe uharibifu uliopo kiasi kwamba taka taka zinashindwa kufikishwa sehemu husika jinsi dampo lilivyoharibika, viongozi wa wa dampo hili  wanahusika moja kwa moja kwani badala ya kutoa maelekezo ya umwagaji mzuri wa taka wao wanaruhusu taka kumwagwa njiani, nimemwagiza bwana  afya hili swala alishughulikie na wale wote waliohusika nitawachukulia hatua " Amesema Sheilla.

Amesema kilichomsikitisha zaidi ni kwamba mtambo wa gari taka ni la Manispaa na mafuta wanatoa Manispaa laikini hakuna hata pesa na chanzo chochote cha mapato  wanachokipata jambo ambalo hawezi kulivumilia huku akimtaka bwana afya kuwa mkali la sivyo wote watawajibishwa kwa mujibu wa sheria na matumizi mabaya ya mali za Umma.

Katika hatua nyengine amesema kama bwana afya hata kuwa mkali kwa hilo na kushindwa kuchukua hatua atatafuta mwenyewe walinzi watakao kuwa wanalinda na kuweka Uongozi utakaokuwa na maslahi kwa Manispaa na kuchangia mapato kwa ajili ya maendeleo.

Naye Afisa Mazingira Manispaa ya Morogoro, Samwel Subi, amesema wamepokea ushauri wa Mkurugenzi wa kusimamisha shughuli zote za uchimbaji Vifusi.

Pia amesema kuwa, kwa sasa wanakabiliwa na changamoto za kuharibikiwa na mitambo miwili ya magari ya taka ambapo baada ya Mkurugenzi kutoa maelekezo wameshaanza kuyatengeneza na wana amini baada ya ya matengenezo hayo kero za taka zitakuwa zimetaturiwa na kuwaondolea wananchi kero ya moshi, harufu mbaya pamoja na kuazliana kwa nzi.

Amesema kwa Sasa Manispaa ipo katika mchakato wa kutengeneza Dampo la Kisasa baada ya kupata eneo jipya Mkundi ambapo wapo katika mpango wa kulipa fidia kwani Dampo  hilo kwa sasa lipokaribu na makazi  ya watu hivyo kusababisha kero kwa wananchi.

Kuhusu uchimbaji wa Vifusi katika dampo hilo,amesema wameshatoa maelekezo kwa Meneja wa Dampo kwamba yeyote atakayeonekana anachimba kuchukuliwa hatua za kisheria.

"Tumeshaongea na wananchi, Uongozi wa Mtaa pamoja na Mhe. Diwani wa kata hii ya Mafisa kwamba kama wataona mtu yeyote anachimba vifusi watoe taarifa kwa ajili ya utekelezaji wa kumchukulia hatua za kisheria,  na kama ni mtumishi hatua za kinidhamu zitachukuliwa" Amesema Subi

Amesema kuwa Vifusi vilivypo vitumike katika kufukia takataka katika dampo hilo, ili ziweze kuoza kwa urahisi na kuzuia nzi wasiendelee kuzaliana.

Kwa upande wa Mkazi wa eneo hilo, Yusuph Abdallah amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa hatua aliyochukua ya kupiga marufuku uchimbaji wa vifusi pamoja na kufuatilia maendeleo ya dampo hilo.

Amesema Uongozi wa Dampo hauwatendei haki kabisa kwani taka zimezagaa hovyo kiasi kwamba zinapelekea magonjwa ya milipuko.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.