Header Ads

Wadau wakutana kujadili utekelezaji wa shughuli za VVU Manispaa ya Morogoro na kutoa taarifa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2019.




Mratibu wa kudhibiti Ukimwi Manispaa ya Morogoro, Upendo Elias, akiwa katika mkutano wa Kamati ya kudhibiti Ukimwi ya kutoa taarifa ya takwimu ya utekelezaji katika kipindi cha miezi 3 ya huduma za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa Mama kwenda kwa Mtoto kipindi cha Septemba, Oktoba na Novemba 2019.
Dkt Lebby
KIKAO cha Wadau kujadili utekelezaji wa shughuli za VVU kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2019 kimetoaa taarifa hizo leo mara baada ya kukutana katika Ukumbi wa Manispaa ya Morogoro leo Januari 29, 2020.

Katika kikao hicho kimetoa takwimu ya utekelezaji katika kipindi cha miezi mitatu ya huduma za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa Mama kwenda kwa Mtoto kipindi cha Septemba , Oktoba na Novemba 2019.
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias akifafanua jambo wakati wa kutoa taarifa za ukatili wa kijinsi na ukatili dhidi ya watoto leo.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mratibu wa kudhibiti UKIMWI Manispaa Upendo Elias, amesema huduma ya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto katika Manispaa ni endelevu huku wakina mama wajawazito wakipatiwa ushauri nasaha juu ya upimaji wa VVU na kupatiwa dawa pale wanapogundulika wameambukizwa VVU.
Wadau wa maendeleo ya mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI wakifuatilia kwa umakini mkutano wa uwasilishaji wa Taarifa ya kuzuia na kupambana na VVU na UKIMWI  kipindi cha miezi 3 Septemba, Oktoba na Novemba 2019.

Amesema mpaka sasa wakina mama wajawazito wamekuwa na muitiko mzuri katika upimaji wa VVU na kujitokeza kwa wingi kupima lakini na wale waliokutwa na maambukizi ya VVU walishauriwa kuleta wenzi wao ili nao wapime VVU lakini mwitiko umekuwa mdogo.


"Bado uhamasishaji unaendelea wa kutoa elimu ili wanaume wawe wanajitokeza kwa wingi kupima afya zao, hususani wale ambao wenzi wao wamepatikana na maambukizi" Amesema Upendo.

Aidha , amesema wajawazito waliopima VVU ni 5088, wenza wao 1590, jumla waliopatikana na maambukizi ni 196 huku wanawake waliopatikana na maambukizi ya VVU 112 na wenza waliopatikana na VVU ni 84 huku jumla ya wakina mama waliopima idadi yao ni 6678.

Mbali na VVU lakini amesema taarifa ya wagonjwa wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU kwa kipindi cha Julai hadi Septemba jumla yao ni 30,421, wanawake chini ya miaka 15 ni 958 na wanawake walizidi miaka 15 na kuendelea ni 20943 huku wanaume chini ya miaka 15 wakiwa 950 na walio zaidi ya amiaka 15 ni  7570.

Amesema elimu ya ushauri nasaha hutolewa kwa wagonjwa wanaotumia dawa na jinsi ya kujihudumia wenyewe na kujikinga na magonjwa nyemelezi.

Pia ametoa taarifa ya idadi ya watu wenye UKIMWI wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU/UKIMWI kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2019, ambapo jumla ya wanaume zaidi ya miaka 15 walikuwa 3292 na chini ya miaka 15 ni 293 huku wananwake zaidi ya miaka 15 8956 na chini ya miaka 15 ni 274 ambapo jumla yake ni 12815.

Mbali na hayo, amesema taarifa hizo zimekuwa zikiandikwa kwa kila robo mwaka ,ambapo taarifa za Oktoba , Desemba 2019 bado ziko kwenye mchakato.

Katika upimaji VVU kwa hiyari katika kipindi cha Septemba, Oktoba, Novemba 2019, idadi ya waliopima Wanawake 7319 na wanaume 5452 aina ya huduma ya VCT/PITC/HBHTC na waliopatika katika huduma hiyo ya vipimo wanaume 339 , wanawake 629 jumla 968 na waliopima VVU kupitia huduma ya PMTCT wanaume 1590, wanawake 5088 na waliopatika na VVU wanaume 84 na wanawake 112 jumla 196 sawa na aslimia 5.9

Amesema kiwango cha maambukizi kimeongezeka kwa asilimia 0.5 ukilinganisha na kiwango cha robo ya kwanza ambapo kiwango kilikuwa asilimia 5.4 huku sababu ya ongezeko hilo ikitajwa kuwa ni uibuaji wa wateja wenye maambukizi kwa kutumia upimaji wa kulenga wateja kwa kuwatafuta wateja wenza walio na maambukizi wanaopata huduma ya tiba na matunzo (index Testing).

Pia katika taarifa ya magonjwa ya ngono Manispaa ya Morogoro kwa mwezi Septemba , Oktoba na Novemba 2019, kutokwa uchafu sehemu za siri wanaume  141, wanawake 336 jumla 477, vidonda sehemu za siri wanaume 37 , wanawake 32 jumla 69, maumivu ya nyonga wanawake 403, magonjwa ya ngono mengineyo wanaume 269 na wanawake 941 jumla 1210 jumla kuu wanaume 269 na wanawake 941 na kufanya kuwa 1210.

Katika upande wa Tohara kinga kwa Wanaume na Watoto wachanga kipindi cha Septemba , Oktoba na Novemba 2019 ambapo katika kipindi hicho jumla ya wanaume 151 walifanyiwa tohara na watoto 6 na kufanya idadi ya waliotahiriwa kuwa 157.

Katika utoaji huduma , amesema Manispaa imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali katika mapambano ya VVU na UKIMWI ikiwamo , JSI, THPS, JHPIEGO, BORESHA AFYA,KONGA, My Health Foundation, MOSAPORG, HACOCA, Care Youth Foundation na UMATI 

Amesema Kamati ya Ukimwi mahala pakazi ilikaa kikao tarehe 11/1/2020 pamoja na masuala mengine yaliyojadiliwa taarifa ya hali halisi ya maambukizi ya Manispaa ya Morogoro ilijadiliwa na tahadhari ilitolewa kwa watumishi kuchukua tahadhari kwani maambukizi yapo juu.

Naye Afisa  Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina  Mathias, amesema licha ya maambukizi ya UKIMWI lakini Manispaa ya Morogoro imekuwa ikikumbwa na suala zima la ukatili wa kijinsia hususani ukatili dhidi ya Watoto wadogo.

Amesema kwa upande wa watoto matukio ya ukatili wa kimwili, ikiwamo vipigo , kuchomwa na kitu chenye ncha kali jumla ya watoto 6 wakiwemo wanaume 6 wamefanyiwa vitendo  na ukatili wa kingono ikiwamo kubakwa na kulawitiwa watoto 13 wakiume 3 na wakike 10 wamefanyiwa vitendo hivyo na kesi 5 zipo mahakamani.

Licha ya takwimu hizo lakini kitengo cha Ustawi wa Jamii hakina Ofisi ya kufanyia kazi hivyo kupelekea maadili ya taaluma kukiukwa na utendaji kazi kuwa mgumu kutokana na kukosa usiri kwa wateja kwani ofisi inayotumika ni moja kwa watumishi wa kada mbalimbali wa idara ya afya.

"Tunafanya kazi nzuri sana , hivyo namuomba Mkurugenzi wetu wa Manispaa atupatie Ofisi ili wateja wetu waweze kuwa huru kujielezea na kuficha siri (faragha) wakati wa kuwahudumia jambo ambalo kwa sasa tunakosa na kutengewa bajeti ambayo itasababisha utekelezaji kuwa na ufanisi unaozingatia kanuni na taratibu za Ustawi wa jamii" Amesema  Sidina 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.