WAZIRI JAFO AIPONGEZA MANISPAA MOROGORO KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.
WAZIRI wa
Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani JafO, ameipongeza Halmashauri ya
Manispaa ya Morogoro, kwa utekelezaji na usimamizi bora wa Miradi ya maendeleo
hususani ilie ya Kimkakati.
Pongezi hizo
amezitoa leo Januari 21, 2020 wakati wa sherehe ya Uzinduzi wa Shule ya
Sekondari ya Mji Mpya iliyopo Kata ya Lukobe.
Akizungumza
na Waandishi wa habari, Mhe. Jafo, amesema kuwa katika Mkoa wa Morogoro ni
Manispaa ya Morogoro pekee imekuwa ikitekeleza maagizo yake kwa ufanisi wa hali
ya juu jambo lililomfanya azidi kuisifia miradi pamoja na Uongozi wa Manispaa
ikiwamo Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Manispaa.
Amesema
hatua iliyofikia shule hiyo hadi inazinduliwa ameridhika nayo kwa asilimia 100
na kuwaomba viongozi waendelee kuchapa kazi na kufuata maelekezo ya Viongozi
wao wajuu wanapotoa matamko ya kiutendaji.
Aidha
amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Rais Dkt John Magufuli, katika
mwaka januari 2016 , imekuwa ikitumia takribani Bilioni 23.86 kila mwezi kwa
ajili ya elimu bure ,ambapo mwaka 2019 Septemba Bilioni 968 zilipelekwa Mamlaka
za Serikali na Bilioni 203.6 zilitumika kwa ajili ya miundombinu ya Shule.
Amesema pesa
zote zinazotekeleza miradi mikubwa hapa nchini zimetokana na nguvu ya Rais
katika ukusanyaji wa kodi .
Amesema
Serikali awali ilikuwa ikiusanya kodi ya Shilingi Bilioni 800 huku ongezeko
hilo likizidi kupaa na kufikia Trioni 1.3 hadi Trioni 1.9 ni zaidi ya ongezeko
la kodi la kihistoria lakini pesa zote zimekuwa zikielekezwa katika miradi ya
maendeleo.
"Nimeridhika
sana na shule hii, nataka ujenzi huu uwe mfano kwa Wakandarasi wengine kwani wamefanya kazi nzuri na kwa wakati,
lakini niwaonye wale wanaokusanya pesa
za Seriklai mtaani wairudishe haraka pesa hizo sio mali zao ni za
Serikali, tukiwa na mapato makubwa ndivyo tunavyozidi kutekeleza miradi mikubwa
kwa ubora wenye viwango vinavyoendana na thamani ya fedha, nawapongeza sana
Manispaa ya Morogoro hamkuniangusha mnafanya vizuri sana katika miradi
yenu" Amesema Jafo.
Amesema
baada ya uzinduzi wa Shule hiyo, kilichobakia ni Uongozi kupambana na ufaulu wa
elimu kwani zaidi ya Wanafunzi Elfu 83
waliofaulu viwango vya madaraja (i-iii) katika matokeo ya kujiunga na kidato
cha tano wanatoka katika Shule za Serikali.
Wakati huo
huo amepiga marufuku Walimu wanaofundisha katika Shule za Serikali kuacha tabia
za kukatiza vipindi kwenda kufundishi shule
binafsi ambapo wakigundulika watachukuliwa hatua za kisheria.
Pia ametoa
agizo kwa Maafisa Elimu wa Msingi na Sekondari, kuhakikisha wanapita kila shule
na kuangalia walimu wakuu waliodumu kwa miaka 5 hadi 15 bila mafanikio ya madaraja
ya juu ya ufaulu washushwe vyeo na kuwa walimu wa kawaida.
Kuhusu Afya,
Waziri Jafo, amesema kwa miaka mitano chini ya Mhe. Rais Dkt John Magufuli ,
wametengeneza vituo vya afya 352 kutoka vituo 118 huku mwaka huu wa fedha
wametenga bajeti ya vituo 52 na kufanya vituo hivyo kuwa 404 nchi nzima.
Pia
wametengeneza jumla ya Hospitali 67 za
Wilaya na kuongeza 3 ambapo mwaka huu wa fedha
wametenga pesa kwa ajili ya kuongeza Hospitali 27 za Wilaya.
Naye, Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Mhe.Loata Sanare, ameipongeza Serikali ya awamu ya tano
chini ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, kwa kuwapatia fedha za ukarabati wa
Shule kongwe pamoja na miundombinu ya
ujenzi wa Maboma 24 katika shule 12 za Sekondari Manispaa ya Morogoro .
Miongoni mwa
Shule Kongwe zilizopatiwa fedha za ukarabati ni pamoja na shule ya Sekondari
Morogoro, Kilakala .
Amesema
Shule za Sekondari za Serikali katika Mkoa wa Morogoro zipo 184 na binafsi zipo
63.
Amesema ili
kufikia viwango vya ufaulu wamewekeana mikakati na waalimu wote wakuu wa
morogoro huku miongoni mwao wakishindwa kufikia makubaliano waliyokubaliana
watashushwa madaraja na kuwa walimu wa kawaida.
"Haiwezekani
Serikali inatumia mabilioni ya fedha harafu tunapata matokeo mabaya, lazima
tukimbizane na kupeana mikakati mizito nahisi maamuzi ya kushushwa madaraja
yatapelekea walimu wakuu kujituma na kupata matokeo mazuri, tuwe na uchungu na
hizi fedha za wanyonge tusiibie serikali yetu kwakuwa bila kufika malengo ni
sawa na kumwibia mwajiri wako fedha"Amesema RC Loata.
Hata hivyo
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe Regina Chonjo amesema watafanya kazi usiku na
mchana kuhakikisha matokeo ya ufaulu kwa wanafunzi yanakuwa makubwa na Wilaya
ya Morogoroinaongoza katika ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ijayo.
Pia
amewataka waalimu wakuu wasimamie miundombinu ya shule kwani fedha zinazowekezwa
katika miradi ya elimu ni mikubwa sana.
Mbunge wa
Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, amesema shule zitakazo ongoza
kuingia 10 bora katika Manispaa ya Morogoro atatoa zawadi ya Shilingi Milioni
10.
Amemuomba
Mhe. Jafo kufikilia miundombinu ya barabara za kata tatu zinazoizunguka Shule
ya Sekondari Mji Mpya pamoja na kuweka mazingira ya upatikana ji wa Maji .
Pia Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amesema licha ya uzinduzi wa
shule hiyo lakini bado manispaa imekuwa ikitekeleza miradi mikubwa ya maendeleo
ikiwamo mradi wa Soko jipya la Kisasa, Stendi Mpya ya daladala.
Pia
amemuomba Mhe. Jafo kulifanyia kazi agizo laMhe. Rais Dkt. John Magufuli baada
ya kutoa tamko la Stendi ya Msamvu kurudishwa Manispaa lakini hadi leo tamko
lake halijatekelezwa.
Post a Comment