LAAC YAIPONGEZA MANISPAA YA MOROGORO KWA USIMAMIZI MZURI WA MRADI WA SOKO KUU LA KISASA NA KUTOA USHAURI JUU YA USIMAMIZI BORA WA MAKUSANYO YA FEDHA.
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imeipongeza Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro kwa utendaji mzuri wa kusimamia ujenzi huo pamoja na kuweka mikakati thabiti ya ukusanyaji wa mapato.
Pongezi hizo zimetolewa leo Januari 10,2020, na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Vedastus Ngombale ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, baada ya kamati hiyo kufanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa Soko Kuu la kisasa pamoja na kupitia ripoti ya mradi huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mkoani Morogoro Mhe. Vedastus, amesema kasi ya mradi huo imewafurahisha hivyo ameitaka Manispaa kuhakikisha sehemu iliyobakia ya ujenzi inakamilika kwa wakati uliopangwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mhe. Vedastus Ngombale (kulia) akisikiliza kwa makini hoja za wajumbe wa kamati na Wataalamu wa Manispaa ya Morogoro. |
Amesema kuwa, Manispaa ya Morogoro inahitaji kupongezwa sana kwani kabla ya pesa za ruzuku ya Serikali katika Miradi Mikakati tayari Halmashauri ya Manispaa ilishaanza kutafuta pesa kwaajili ya ujenzi , hizi ni juhudi kubwa sana , hatua iliyofikia ya mradi imeonesha thamani ya pesa iliyotumika japo kuna mapungufu madogo madogo lakini naimani watakaa na kuyaweka sawa .
Amemshauri Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro pamoja Mkurugenzi wa Manispaa kuhakikisha kwamba mara baada ya kukamilika kwa mradi wa Soko kuu la kisasa waweke uongozi mzuri ambao wataamua katika Baraza lao na utakaokuwa unauwezo wa kukusanya fedha ili Manispaa iweze kuendesha miradi mingine.
"'Niwapongeze viongozi wa Manispaa kazi inaonekana fedha kidogo kazi kubwa , kwakweli mradi huu tutautangaza kwa Mhe. Rais Dkt . John Magufuli kuonesha jinsi gani mlivyokuwa makini katika matumizi ya fedha, pia niwaombe mjifunze katika miradi ya wenzenu ili muweze kuendesha soko vizuri, isije tena mkawa mmeleta mradi harafu mradi huo ukaleta migogoro na kutokuwa na tija kitu ambacho hakitawasaidia katika kufikia malengo yao ya kukusanya kodi kwani tunayo mifano mbalimbali ya miradi kukamilika lakini imekuwa haina tija hii ni kutokana na usimamizi mbovu, sasa hivi tumekuja kuangalia maendeleo ya mradi lakini tutakuja tena kuangalia namna mradi huo unavyoendeshwa niwaombe mzingatie sana ushauri wa kamati ya Bunge ili mradi huo ufanye kazi ipasvyo ili usije kutia hasara kwa Manispaa na Serikali.
Hata hivyo, amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, kuhakikisha mara baada ya kukamilika kwa mradi wa Soko kuu la kisasa waweke uongozi mzuri ambao wataamua katika Baraza lao na utakaokuwa unauwezo wa kukusanya fedha ili Manispaa iweze kuendesha miradi mingine.
Katika hatua nyengine, ameutaka Uongozi wa Halmashauri kuhakikisha wanaweka viwango vya bei rafiki na nafuu kwa Wafanyabiashara ili waweze kufanya biashara katika kupata vipato vyao na Halmashauri kuingiza mapato.
Amesema Mhe. Rais Dkt John Magufuli hanaga utani katika fedha anazozitoa katika miradi , hivyo anataka kuona pesa anazozitoa zinatumika kwa miradi iliyokusudiwa na kuleta tija kwa Wananchi na kuona watu wa chini wananufaika na miradi hiyo.
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa LAAC na Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mtwara,Mhe. Abdallah Chikota , ameshauri Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, kujiandaa vyema kupokea mradi huo wa soko.
Amesema kuwa, mradi huo ni mkubwa lazima wahakikishe wanaunda timu ndogo ya Wataalamu ili mradi usiishie kati kwa ajili ya kuendesha Soko hilo au kuajiri hata kwa muda wataalamu kutoka nje badala ya kumtegemea Afisa Biashara jambo ambalo watashindwa kufikia malengo.
Pia amewashauri Mwanasheria pamoja na watu wa uchumi Manispaa waangalie miongozo ya fedha kutoka katika Wizara ya fedha ili kuona gharama na makusanyo wakati wanakwenda kuandaa mikataba ya uendeshaji wa Soko hilo.
Pia katika upande wa maegesho ya magari ameshauri wasiangalie makusanyo waangalie gharama za makusanyo kwani mradi huo ni wawanchi wakifanya bei kubwa watawakimbiza wateja na watakosa watu wa kuwaingizia mapato.
Hata hivyo, Mbunge wa Viti maalumu Mtwara Mjini, Mhe. Tunza Malapo, ameitaka Manispaa kuangalia upya suala la tozo za maegeshho kutoka Shilingi 3000/= kwani bei hiyo ni kubwa na ukizingatia mradi huo ni wa wananchi.
Amesema athari ya kuwa na bei kubwa kutafanya iwakimbize wateja na kutafuta mahala pengine kwa ajili ya kupata huduma lakini manispaa itakosa watu na malengo waliyojiwekea ya makusanyo hayatakwenda kama wanavyotarajia.
Katika hatua nyengine, Mjumbe wa kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo la Mbagara Wilaya ya Temeke Jijini Dar Es Salaam, Mhe. Issa Mangungu ametoa ushauri kwa Uongozi wa Manispaa hiyo kuhakikisha mifumo ya zimamoto inaimarishwa kwakuwa mradi huo ni mkubwa na umetumia pesa nyingi kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.
Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, ameupongeza Uongozi wa LAAC kwa kutembelea mradi wa Soko kuu la kisasa na kujua maendeleo yake.
"Katika mradi huu katika kuupokea tumeshirikiana na wadau na wale wafanya biashara ambao walikuwa wakifanya biashara katika Soko la zamani tuliwaondoa na kuwapeleka soko la manzese na mitaani lakini kwa mikataba ili tutakapo maliza soko letu vipaumbele vya kwanza vitakuwa ni wao na mambo mengine baraza la madiwani tutakaa na kuona ni utaratibu gani wa kuwaingiza wafanyabiashara wengine' Amesema Sheilla.
Aidha amesema atahakikisha mara baada ya kukamilika kwa mradi huo, wafanyabiashara waliosaini mikataba ya awali kabla ya ujenzi kuanza ambao walikuwa katika Soko la zamani wanapewa kipaumbele kufanya biashara katika soko hilo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, ameishukuru LAAC na kusema wamefanya jambo zuri kutembelea mradi huo.
Amesema, kitendo cha LAAC kutembelea miradi mbali mbali kinasaidia kuzimulika Manispaa na kuonesha jinsi utekelezaji wa miradi inavyotekelezwa pamoja na kuona thamani ya fedha inavyotumika .
Mhandisi wa Manispaa, Juma Gwisu amesema mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 85 na wanatarajia hadi kufkia Februari 20 , 2020 mradi huo utakuwa umekamilika.
Post a Comment