Header Ads

Picha na matukio mbali mbali ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi kilivyotembelea Manispaa ya Morogoro

Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, akipokea tuzo waliyopewa Manispaa ya Morogoro  kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Dkt. Lucy Shule wakati wa ziara kwenye Ukumbi wa Manispaa ya Morogoro.
Wakufunzi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wakiwasili Manispaa ya Morogoro mapokezi hayo yalifanywa na Afisa Habari Manispaa ya Morogoro, Lilian Henerico.




Mkurugenzi wa Mafunzo Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Dkt. Lucy Shule akitoa utambuloisho kwa wakufunzi na viongozi alioambatana nao katika ziara hiyo ya kujifunza namna ya ukusanyaji wa Mapato katika Manispaa ya Morogoro. 
Afisa Habari Manispaa ya Morogoro, Lilian Henerico akielezea na kuwasilisha taarifa juu ya taswira ya Manispaa ya Morogoro mbele ya wageni.



Mchumi Manispaa ,Rubeni Urasa, akielezea mipango ya Bajeti ya Manispaa ya Morogoro.

Afisa Mapato,  Manispaa ya Morogoro , Muhusini Mhina , akielezea jinsi manispaa inavyoweza kukusanya mapato na vyanzo vya mapato vilivyopo katika Manispaa hiyo.









Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba akipokea tuzo kwa Kaimu Mkurugenzi Ofisini kwake mara baada ya  Chuo cha Taifa cha Ulinzi kutoa tuzo hiyo kufuatia kuridhishwa na mapokezi pamoja na taarifa nzuri iliyowasilishwa juu ya ukusanyaji wa mapato na vyanzo pamoja na miradi .

Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba,  akiwa na tuzo kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi.
Miongoni mwa Wakilishi waliofika katika ziara hiyo kutoka chuo cha Taifa cha Ulinzi ni pamoja na Tanzania, Kenys, Burundi, Msumbiji, Nigeria, pamoja na Misri.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.