Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro amewataka Watendaji wote kuacha kukaa Ofisini na badala yake washuke chini kuwasikiliza wananchi
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewataka viongozi na watendaji wa Manispaa ya Morogoro kushughulika na matatizo yanayowakabili wananchi,na kuwaasa baadhi yao wasiotimiza wajibu wao kufanya kazi.
Akizungumza na Waandishi wa habari, amewataka watendaji kata, Mitaa, Wenyeviti wa Mitaa , Madiwani na wakuu wa Idara zote katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, kuhakikisha wanatenda kazi ipasavyo.
Amesema lengo la Ziara hiyo ni kutatua kero zinazowakabili wananchi, huku akisema kuwa mlundikano wa kero zilizopo mtaani zinatokana na kutowajibika kwa Watendaji wa ngazi ya chini.
Amesema hataki kuona tena Kero hazitatuliwi katika ngazi za chini ambapo zinaweza kusikizwa na Mtendaji wa mtaa, Mwenyekiti wa mtaa, Mtendaji kata,au Afisa Tarafa.
" Viongozi nawaomba mtatue hizo kero ili kuendana na Kasi ya Mhe.Rais Magufu ya kufanya kazi kwani hapa kazi tu na kuweza kuendana na Ilani ya Chama inatutaka tufanye kazi za kuwasikiliza Wananchi " Amesema Sheilla.
Katika Ziara hiyo amesema zipo Kero zilizopata ufumbuzi papo kwa papo na nyingine zilizochukuliwa na kupelekwa katika ngazi husika ambapo Ni katika hataua mbalimbali za kutafutia Ufumbuzi.
Aidha katika Mgogoro wa Afya amataka wauguzi Pamoja na wafanyakazi katika sekta ya Afya wanaotumia lugha mbaya na chafu kwa wagonjwa kuacha tabia hiyo vinginevyo watachukukiwa Hatua.

Amesisitiza kuwa viongozi watakaoona kwamba hawawezi kuendana na kasi hiyo, kwa kuwasikiliza wananchi, kutatua kero zao pamoja na kutotimiza majukumu yao ipasavyo, wajitoe wakafanye kazi nyingine kabla ya kusimamishwa kazi huku akieleza kuwa wananchi wengi hawasikilizwi kero zao na kwamba kero kubwa waliyokutana nayo ni migogoro ya ardhi.
Alifafanua kuwa viongozi wa mitaa na Kata wamekuwa chanzo cha migogo hiyo kwa kuwasaidia wavamizi kuchukua maeneo ya wananchi ambapo wamekuwa wakiwagongea mihuli ilhali wanafahamu kuwa sio maeneo yao.
Amesema lengo la Serikali za mitaa ni kusogeza huduma karibu na wananchi na Kila kiongozi katika ngazi mbalimbali aliyechaguliwa, kuteuliwa au kuajiriwa anapaswa kishughulika na matatizo ya wananchi.
Mkurugenzi ame sema kuwa malengo ya manispaa hiyo ni kudumisha amani, utawala bora na kufikia maendeleo endelevu.
Aidha amesema wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaongeza mapato ya ndani kupitia Vyanzo vipya vya mapato, ikiwamo Miradi ya Kimkakati kama vile Soko Kuu la Kisasa linalojengwa kwa shilingi Bilioni 17, Stendi ya Mabasi Msamvu, Stendi mpya ya Daladala ili kukusanya mapato na kufikia bilioni 10 na kuendelea kwani kwa sasa mapato ya ndani ni Shilingi Bilioni 6.7.
Amesema kuwa Manispaa kupitia fedha za mkopo wa Benki ya Dunia chini ya fedha za uboreshaji Miji (Urban Local Government Strengthening Program ULGSP) IMETENGA JUMLA YA sHILINGI milioni 774 kwa ajili ya ujenzi wa Mto Kikundi ambao ulikuwa unaleta madhara kwa Wananchi pindi Mvua zinaponyesha.

Katika hatua nyingine amewataka watendaji wa Kata na Mitaa kufanya vikao angalau Mara moja kwa mwezi ili yeye akiwa katika ziara zake akutane na Kero za maendeleo tu na zile ndogo ziwe zimetatuliwa na Watendaji hao.
Kuhusu kutokukamilika kwa baadhi ya miradi, amesema wale wakandarasi waliopewa Pesa za Serikali na Manispaa kama hawajamaliza miradi kwa wakati watamalizia kwa Pesa zao na kuwataka kukamilisha kwa wakati ili kuupunguza changamoto zinazowakabili wananchi.
Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Mafisa , Mhe. Daud Salum Mnadi, amemuomba Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, kuwasaidia katika kukamilisha Kituo cha Afya cha Mafisa, Soko , Shule pamoja na kukarabati barabara.

"Mkurugenzi Kituo chetu cha afya kilikuwa kinatoa huduma za Mama na Mtoto lakini baada ya kukatiwa maji hadi leo huduma hizo zimekata, tunakuomba utusaidie ili huduma hizi ziendelee kupatikana hapa, ukiangalia upande wa barabara hazipitiki hivyo kwa kikao hiki kilichotukuka naimani haya tuliyokueleza mbele ya hadhara utayafanyia kazi na kutatua changamoto zetu ili wananchi hawa waone jinsi tunavyopambana na matatizo yao nakuendelea kutuamini tena kuwaongoza katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka huu 2020" Amesema Mhe. Mnadi.
Pia Mkurugenzi amewaagiza Afisa Mazingira pamoja na TARURA wasimamishe haraka zoezi la uchimbaji wa Kifusi kilichopo Dampo la Kata ya Mafisa hadi pale watakapomletea kibali kilichowaruhusu kuwezo kuchimba katika eneo hilo.
Katika hatua nyingine, amesema tatizo la kuchelewa uzoaji wa taka taka , linatokana na uzembe wa wakandarasi waliochukua tenda na kuwa na uwezo mdogo wa kutokufanya kazi kwa usahihi na kuahidi kubadilisha mfumo wa kuwaondoa na kutangaza tenda mpya kwa makampuni yenye uwezo wa kufanya kazi.
Mstahiki meya wa Manispa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amempongeza Mkurugenzi kwa kushirikiana na timu ya Wataalamu wake wakuu wa idara pamoja na wakuu wa Taasisi za Serikali kwa kuwafuata wananchi jambo ambalo linawafanya Wananchi waweze kuwa na imani na kuwaaminisha kwamba Serikali yao ni Serikali ya kazi kweli.
Naye Mkazi wa Kata ya Mafisa, Steven Banda, amesema barabara mbovu kiasi cha kusababisha magari kutokufika na watoto wanapata tabu ya usafiri na wazazi wanatumia pesa nyingi kumfikisha mtoto shule kwa kupanda bodaboda.
Kibibi Hussein mkazi wa Kata ya Kihonda maeneo ya Kilimanjaro amesema kuwa Shule ya Msingi Noto inawanafunzi wengi sana hivyo wanataka kuoneshwa maeneo ya wazi ili wananchi waweze kujitolea kwa ajili ya ujenzi wa shule nyengine.
Swala la nauli nalo liliibuka huku wananchi waishio manyuki, Azimio kulipa nauli shilingi 400 wakati wa kwenda mjini na wanaporudi nyumbani wamekuwa wakitozwa shilingi 500 ambapo Mkurugenzi amewataka watu wa Sumatra kulichukua na kuhakikisha wanakaa na wamiliki wa magari ili changamoto hiyo iweze kuondolewa na wale watakao kaidi wananchi wachukue namba zao za magari walifikishe SUMATRA.
Miongoni mwa kero zilizojitokeza ni pamoja na Bima ya afya, elimu, usafiri, barabara, soko, mazingira, MKURABITA, ardhi, NIDA, n.k.
Ikumbukwe kwamba huo ni mwanzo lakini mikutano hiyo ya hadhara ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi itakuwa ni endelevu kwa kata zote 29 zilizopo Manispaa ya Morogoro.
Ikumbukwe kwamba huo ni mwanzo lakini mikutano hiyo ya hadhara ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi itakuwa ni endelevu kwa kata zote 29 zilizopo Manispaa ya Morogoro.
Post a Comment