NEMC kutowavumilia Wazalishaji, uingizaji na matumizi ya mifukombadala aina ya Non-Woven isiyokidhi viwango vya 70 Gram Per Square Metre (GSM)kutumika nchini.
Afisa Mazingira Mwandamizi na Mkaguzi wa Mazingira, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Abella Mayungi akiwa katika msako. |
BARAZA la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) , wamesema kamwe hatakuwa tayari kuwavumilia Wazalishaji , Waingizaji wa Mifuko mbadala isiyokidhi viwango vya 70 Gram Per Square Metre (GSM)kutumika hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Afisa Mazingira Mwandamizi na Mkaguzi wa Mazingira, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Abella Mayungi wakati wa kuhitimisha zoezi la msako wa mifuko hiyo katika Manispaa ya Morogoro leo Januari 24,2020.
Muuza duka akisaini fomu ya faini na maelezo baada ya kukutwa na mifuko ya plstiki . |
Amesema kuwa wapo Wafanyabisahara wasio waaminifu kutaka kuingiza mifuko isiyokidhi viwango aina ya Non-Woven na kujikuta kila uchwao wakizidi kutengeneza na kusambaza mifuko hiyo kinyume na sheria.
“Kumeanza kujitokeza uvunjifu wa sheria katika uzalishaji na uingizaji wa mifuko mbadala aina ya non-woven. Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeweka vigezo vya mifuko mbadala aina ya non-woven inayoweza kutumika nchini ikiwa ni pamoja na Uzito usiopungua GSM 70 (Gram per Square Metre), iweze kurejelezwa, Ioneshe uwezo wa kubeba, anuani ya mzalishaji naiwe imethibishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)” amesema Mayungi.
Amefafanua kuwa malighafi inayotumika na Viwanda vya ndani imekuwa ikipelekwa nje, hivyo Serikali imeweka masharti magumu kwa lengo la kulinda viwanda vya ndani na kuruhusu kusafirishwa kwa malighafi ambayo haitumiki hapa nchini.
Siku ya tano ya Ukaguzi na msako mkali wa kutembelea maeneo mbalimbali kwa ajili ya kubaini mifuko mbadala isiyokidhi viwango pamoja na mifuko ya plastiki ambayo bado inaendelea kutumika ambapo leo NEMC kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Morogoro pamoja na Maafisa wa Halmsahuri ya Manispaa ya Morogoro wamehitimisha zoezi hilo.
Post a Comment