Header Ads

Afisa Mwandikishaji Jimbo la Morogoro Mjini ataka zooezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura liendeshwe kwa kuzingatia sheria na kanuni za TUME.


Afisa Mwandikishaji Jimbo la Morogoro Mjini , Sheilla Lukuba, akifungua semina ya Mafunzo kwa BVR Operators na Waandikishaji wasaidizi katika Ukumbi wa Mount. Uluguru.

AFISA Mwandikishaji wa Jimbo la Uchaguzi Morogoro Mjini  , Sheilla Lukuba, amewataka BVR Operators na Waandikishaji wasaidizi    kuendesha  zoezi hilo kwa mujibu wa Sheria , Kanuni pamoja na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Morogoro Mjini, Sheilla Lukuba (katikati), Kushoto Kamishina wa Tume ya Uchaguzi, Marry Longway (Jaji Mstaafu), kulia ni Mwalimu Mohamed Chambili, Mwenyekiti wa Semina kwa upande wa wawakilishi wa wanamafunzo.
Ameyazungumza hayo, wakati wa Ufunguzi wa Semina ya mafunzo ya Uandikishaji ya BVR Operators na  Waandikishaji wasaidizi  katika ukumbi wa Mount. Uluguru uliopo  Manispaa ya Morogoro leo Januari 31,2020.
Afisa wa Jimbo la uchaguzi la Morogoro, Waziri Kombo akiwa katika semina.
Akizungumza na Waandishi wa habari, amewapongeza washiriki wote walioteuliwa na Tume kuendesha na kusimamia zoezi hilo muhimu la Uandikishaji wa Wapiga kura.
Afisa Uchaguzi Manispaa ya Morogoro, Pendo Chagu akitoa maelekezo wakati wa semina.
Amesema kuwa mafunzo ya jinsi ya kutumia mfumo wa Uandikishaji yanalenga kuwawezesha BVR Operators na Waandikishaji Wasaidizi ili  kupata uelewa wa jinsi ya kutumia kwa ufasaha BVR Kit kwa ajili ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura ili waweze kutoa mafunzo hayo kwa BVR Kit -Operators na Waandishi Wasaidizi ambao ndio wahusika wa  uandikisjaji wa wapiga kura vituoni.

"Matumani yangu baada ya mafunzo haya kila mmoja wenu atapata elimu ya kutosha itakayomwezesha kutekeleza wajibu na majukumu yake katika kufanikisha zoezi hili muhimu, pia nahakika baadhi yenu mlibahatika katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura lililofanyika kwa mara ya kwanza katika mfumo huu wa sasa wa Teknolojia ya BVR (Biometric Voters' Registration) mwaka 2015 hivyo mna uzoefu katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa zoezi hili" Amesema Sheilla.

Aidha, amewataka wanamafunzo wale waliopata ujuzi kipindi cha nyuma na wale wapya kushirikina na wa kutumia uzoefu walionao kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa , kwa bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hilo na kuwafundisha wenzao ambao hawakuwahi kushiriki katika zoezi lililopita ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Pia amewaambia kwamba Mawakala wa Vyama vya Siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura na watazamaji watazamaji wakati wa zoezi zima la uboreshaji ambao watapatiwa vibali maalum ambavyo vitawaruhusu kuingia katika vituo vya kuandikisha jambo ambalo ni muhimu na litasaidia kuleta uwazi katika zoezi hilo.

"Lazima mtambue kwamba , Mawakala wa Vyama Vya Siasana Watazamaji hawatakiwi kuwaingilia watendaji mnapotekeleza wajibu wenu, hivyo maelekezo zaidi kuhusu suala hili yapo kwenye vitabu vya maelekezo mlivyopatiwa na ni muhimu kuyazingatia ili zoezi letu lifanyike kwa mujibu wa Sheria , kanuni na maelekezo" Ameongeza Sheilla.

Mbali  na melekezo, amewaambia kuteuliwa kwao kumetokana na kuaminiwa hivyo wanauwezo wa kufanya kazi hiyo, kikubwa ni kujiamini na kujitambua na kufuata maelekezo yatakayotolewa na Tume ili waweze kufanya kazi wakati wa zoezi la Uandikishaji  pamoja na kufuata Sheria , kanuni, maelekezo na miongozo.

Amesema Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, imedhamiria kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi mkubwa na kuwataka watendaji kuhakikisha wanayajua na kuyatambua vyema maeneo watakayofanyia kazi ikiwemo miundombinu ya kufikia katika Kata na Vituo.

Hata hivyo, amesema katika kufanikisha zoezi hilo, kunahitajika ushirikianao mkubwa kati ya watendaji wote , Serikali , Vyma Vya Siasa na wadau wengine wote, pia waongeze ushirikiano mzuri wa karibu na Ofisi ya Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Morogoro wakati wote watakapokuwa wanahitaji ufafanuzi au maelekezo katika kazi zao huku akiwatakia kazi njema katika mafunzo yao.

Hata hivyo amechukua nafasi hiyo kuwahamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi katika uandikishwaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kutekeleza haki zao za msingi za kikatiba na hatimaye kwenda kuwachagua Viongozi watakao weza kuwaletea maendeleo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wa Diwani, Mbunge na Rais.

Kwa upande wa Kamishina wa Tume ya Uchaguzi, Marry Longway (Jaji Mstaafu) , amewataka Waandikishaji kuzingatia muda wakazi kabla ya saa  2:00 asubuhi wawe washafika katika vituo ili ifikapo saa 2:00 asubuhi kazi zianze kufanyika  ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi na kuendelea katika kazi nyengine za uzalishaji.

"Lazima ufike mapema, uangalie BVR Kit imefungwa, fomu zako zipo tayari , kalamu yako inaandika vizuri, sio inafika saa 2:00 asubuhi wewe ndio unafika unajisachi mfuko peni haiandiki fomu hazionekani , BVR haijawashwa sio utaratibu lakini najua saa 12 jioni ndio muda wa kufunga kazi lakini lazima uangalie taarifa zako umezipangaje kwahiyo mkifuata hatua zote zoezi letu litakwenda vizuri bila matatizo na wananchi, mawakala wa Vyama Vya Siasa wala watazamaji" Amesema Longway.

Pia amewataka waandikishaji kuhakikisha wanawaandika majina na kuanza nao siku inayofuata kwa wale ambao muda wa kufunga kazi utawakauta wakiwa katika foleni ili kukwepa migongano na migogoro kwa wananchi.

Amesema vipaumbele vitolewa kwa Watu wazima, (Wazee), Watu wenye ulemavu, Wajawazito pamoja na wagonjwa hawaruhusiwi kukaa foleni.

Naye,  Afisa wa Jimbo la uchaguzi la Morogoro, Waziri Kombo, amewapongeza maafisa hao kwa kuaminiwa na kuchaguliwa kuifanya kazi kubwa ya kitaifa ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura. 

Aidha amewataka maofisa hao kuwa wasikivu na kuzingatia mafunzo watakayopewa kuhusiana na uendeshaji wa zoezi hilo. 

Hata hivyo Kombo  amesema hawatamvumilia mtu yoyote atakayekuwa mzembe wakati wa uboreshaji wa Daftari. 

" Kama Manispaa yetu ya Morogoro tunataka tuwe watu wa kwanza kitaifa kuandikisha watu wengi zaidi na hii inawezekana tukiwa na weledi na tukizingatia mafunzo tutakayopewa" Amesema Kombo. 
Waandikishaji wakila kiapo.
Waandikishaji wakiwa katika Semina ya Mafunzo. 
Zoezi la uboreshaji Daftari la kudumu la mpiga kura katika Mkoa wa Morogoro linatarajiwa kuanza katika Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro, Halmshauri ya Mji wa Ifakara, Halmshauri za Wilaya ya Gairo, Kilombero, Kilosa, Morogoro na Mvomero kuanzia tarehe 03 hadi 09 Februari 2020.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.