Mkurugenzi Manispaa Morogoro awapongeza Wazazi kwa kuchangia maendeleo ya shule.
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewapongeza Wazazi
wanaowasomesha watoto wao shule ya Msingi Mkundi kwa kujitoa na kusaidia
maendeleo katika shule hiyo.
Akizungumza leo Januari 6, 2020 mara baada ya kutembelea shule hiyo kwa
ajili ya kuangalia mwitiko wa wanafunzi walioandikishwa kuanza darasa la kwanza mwaka 2020, kufuatia mpango wa elimu bure bila
malipo.
Amesema kuwa, kitendo cha Wazazi hao kuchangia kila mmoja Shilingi elfu 15
na tofali 3 kimetokana na Wazazi hao baada ya kuona wingi wa wanafunzi na
changamoto ya madarasa huku akitaka kitendo hicho kiwe mfano wa kuigwa kwa wazazi wengine ikiwa ni mapokeo mazuri ya wazazi kutambua umuhimu wa kusaidiana na
Serikali kwa Maendeleo ya Watoto wao.
"Hii ni hatua nzuri sana, na imeondoa ile dhana ya Wazazi kuachia
Serikali peke yake baada ya kuona elimu inatolewa bure, ndugu zangu kuchangia
sio dhambi, Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, amekuja na mpango wa elimu bure
lakini sio kwamba kila kitu uiachie Serikali kwani elimu ina pembe tatu Mwanafunzi,
Mwalimu pamoja na Mzazi, tukiwa kitu kimoja naamini hata matokeo ya ufaulu wa
watoto wetu utaongezeka na kutengeneza Taifa lenye kuleta matokeo chanya
hususani katika kuelekea uchumi wa kati na Tanzania ya Viwanda" Amesema
Sheilla.
Hata hivyo amesema kuwepo kwa michango shule kumetokana na makubaliano ya wazazi wenyewe kwenye vikao vyao na walimu huku wakipitisha mihutasari katika vikao halali wanavyovifanya katika kuleta maendeleo kwa wanafunzi.
Hata hivyo amesema kuwepo kwa michango shule kumetokana na makubaliano ya wazazi wenyewe kwenye vikao vyao na walimu huku wakipitisha mihutasari katika vikao halali wanavyovifanya katika kuleta maendeleo kwa wanafunzi.
Aidha ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais Dkt John Magufuli kwa kubuni na
kutekeleza mpango wa elimu bure bila malipo, jambo ambalo limesaidia sana
wazazi kuwaandikisha watoto wengi tofauti na kipindi cha nyuma na asilimia
kubwa ya wanafunzi imeongezeka katika uandikishwaji.
Kwa upande wao, Wazazi nao walichukua nafasi ya Kumpongeza Mhe. Rais Dkt.
John Magufuli huku wakisema elimu bure imewasaidia na sasa hivi watoto wengi
wameandikishwa na wanasoma lakini wameomba kuangaliwa kwa jicho la tatu na
kusaidiwa pale watakapo ishia katika jitihada zao za kutatua changamoto
shuleni.
Naye Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Abdul Buhetty, amempongeza
Mkurugenzi kwa kutembelea shule hiyo lakini amemuomba kutatua changamoto zilizopo katika shule za msingi ili kuongeza viwango vya ufaulu na
kuing'arisha Manispaa katika mitihani Kitaifa.
Amesema Shule ya Msingi Mkundi, kabla ya uandikishwaji wa wanafunzi wapya
ilikuwa na jumla ya wanafunzi 2042 na sasa bado zoezi la uandikishwaji
unaendelea.
Mbali na kutembelea Shule ya Msingi Mkundi pia ametembelea Shule ya Sekondari Kihonda Maghorofani.
Post a Comment