MAKALA: Zijue Sifa za Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo ni kiongozi mwenye Ufanisi kazini, kwa kiasi kikubwa, kiongozi huyu amekuwa na uwezo mkubwa wa kuwaunganisha Wana Morogoro katika kufikia maendeleo .
Amekuwa na mamlaka ya kutoa sauti ya kuhamasisha watu kujiwekea dira na utaratibu wa kuifikia dira hiyo. Miongoni mwa sifa zake ni pamoja na uwezo wake wa kuwavuta na kuwashawishi watu makini kutumia vipawa , ujuzi na uzoefu walionao katika kuwezesha kufikia malengo mapana.
Tunaweza kusema mengi yanayohusu wajibu wa mfanyakazi lakini bila kiongozi makini itakuwa vigumu kupata ufanisi unaotakikana. Mkuu wa Wilaya amekuwa ni kiongozi wa Mfano katika Wilaya ya Morogoro kwa utendaji wake uliotukuka mfano amekuwa ni kiongozi anayejua kuibua hamasa kwa watu hivyo kupelekea Utendaji katika Ofisi kuwa wa viwango na wenye tija hususani katika kufuatilia kwa umakini miradi iliyopo katika Wilaya ya Morogoro na kutolea maelekezo ya nini kifanyike katika kufikia malengo.
Ingawa ni kweli tunaweza kuzaliwa na siha ya uongozi, DC Chonjo amekuwa kiongozi makini sana ambaye siku zote za utendaji wake hachoki kujifunza namna bora ya kuwaongoza waliochini yake.
Zifuatazo ni miongoni mwa sifa alizonazo mkuu wa Wilaya ya Morogoro
Kujenga hamasa
DC Chonjo amekuwa na tabia ya kuwafanya watu wakajisikia fahari kufanya kitu bila kusukumwa. Hapa tunazungumzia kuwa na sauti inayosikika mioyoni mwa wale unaowaongoza. Kinyume chake ni kuwatawala watu kwa maana ya kuwalazimisha kufanya kitu wasichojisikia kukifanya.
Unaweza kujenga hamasa kwa namna kadhaa.lakini nilichogundua ni kwamba ni kiongozi ambaye amekuwa akijenga tabia ya kuwafahamu walio chini yake na amekuwa akiwathamini watu wote jambo ambalo limekuwa likiongeza hamasa ya utendaji wa kazi.
Pili, amekuwa kiongozi hodari sana wa kutambua kazi na jitihada zinazofanywa na waliochini yake. Kuna ukweli kuwa zaidi ya mshahara mzuri watu wanatamani kuona kazi wanazofanya zinatambuliwa na kiongozi wao.
Ukijifunza kutambua jitihada za watu wako utawajengea hamasa ya kujituma zaidi.
Kuwa na utaratibu wa kuwaita wale wanaofanya vizuri zaidi utambue kazi zao. mara nyingi amekuwa akiitisha vikao sio tu kwa lengo la kuitisha vikao kuwagombeza watu kwa makosa yao bali kusikiliza maoni yao na kuwapa mrejesho wa kazi nzuri wanazozifanya katika taasisi zao.
Tatu, amekuwa kiongozi mwenye Kujali ndoto za anaowaongoza Moja wapo ya sifa mbaya zinazotajwa kwa viongozi wengi ni tabia ya kupuuza maslahi na mustakabali wa watu wanaowaongoza.
Kuwachukulia watu wako kama mashine zisizo na hisia wala malengo ni namna moja wapo ya kuonyesha unavyowapuuza lakini kwa DC Chonjo hali hiyo imekuwa ni tofauti sana kwake amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kila mkazi wa Morogoro anatimiza ndoto na malengo aliyojiwekea katika kufikia mafanikio ya maisha yake na jamii inayomzunguka.
Pia amekuwa akitambua kwamba sehemu yoyote yenye mafanikio katika taasisi yoyote mafanikio hayo yanachangiwa na bidii ya watu anaofanya nae kazi hivyo kwa kufanya hivyo amekuwa akisababisha kuendelea kuhamasisha watu kufikia malengo ya Serikali anayoingoza katika Wilaya ya Morogoro.
Miongoni mwa kiu kubwa ya kufanikiwa katika kuingoza vyema Wilaya ya Morogoro, ni pamoja na kujali utu wa watu anaowaongoza pamoja na maslahi yao na amekuwa akitengeneza mipango ya wazi ya kuwaendeleza kadri ya uwezo wao ili kuwafanya wana Morogoro au taasisi kufikia ndoto walizojiwekea.
Hata ukiangalia katika ufanyaji kazi wake amekuwa akithamnini watu wake kwa kauli na matendo, pamoja na kuheshimu kazi zao hivyo kuwapelekea Wafanyakazi au taasisi ndani ya Wilaya ya Morogoro kujenga imani kwa kiwango kikubwa juu ya utendaji wake uliotukuka.
Nne, amekuwa Kiongozi anayejiamini hana wasiwasi na kile anachokifanya jambo amabalo linamfanya awe na uhakika kwamba anaiweza kazi yake lakini kujiamini kwake kunatoka na kuwa mvumilivu anaposikia mawazo mbadala na amekuwa hawezi i kuchukulia mawazo tofauti na yako kama uadui na amekuwa kiongozi wa kushauri jambo kwa nia ya kuboresha.
Kadhalika, licha ya kujiamini lakini amekuwa kiongozi mwenye tabia ya kusema ukweli na hadaganyi na amekuwa muwazi kwa Wananchi wake anao waongoza na kuwaambia wale unaowaongoza vile mambo yalivyo hasa katika mazingira kwa ujumla .
Japo sio kazi nyepesi lakini DC Chonjo, amekuwa kiongozi mwenye uwezo na kuwekeza kwenyeweledi na maarifa na mnyeyekevu wa kujifunza na kuwa msikivu kwa Wananchi wake.
Tano, Ujasiri wa maamuzi, DC Chonjo amekuwa kiongozi anayeijua njia bora ya kupita na mwenye uwezo wa kuona mbali na maono mapana yanayoakisi malengo na dira ya taasisi na Wananchi hivyo kumfanya kuwa jasiri wa kuwashawishi waliochini yake kufuata kile anachokiamini katika kufikia malengo.
Siku zote amekuwa Kiongozi Jasiri mwenye uwezo kuthubutu kufanya maamuzi yenye maslahi ya wengi na amekuwa mtu wa kugundua viashiria vya tatizo na kuwaalika wale anaowaongoza a katika kutafuta ufumbuzi hivyo kufanya wale anaowaongoza kuwa na ujasiri wanapoona na wewe kama kiongozi wao anakuwa jasiri na sio muongeaji ni mtu wa vitendo kwa namna anavyoongea , anavyoonekana na jinsi anavyowasiliana na watu.
DC Chonjo amekuwa sio mtu wa kijificha nyakati za matatizo akisubiri wengine watangulie hivyo amekuwa katika mstari wa mbele katika kuamini kile anachokisimamia na kile kinachompa wasiwasi na namna anavyoweza kuonyesha njia katika kufikia mafanikio.
Kwa leo ningependa niishie hapo lakini natumani wasomaji wangu mmepata wasaa wa kumjua zaidi Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo na sifa zake za kiuchambuzi kupitia Chombo huru.
Makala hii ni ya kiuchambuzi na namna ya kumuelezea Kiongozi na kuchambua sifa zake. Tukutane tena siku nyengine Asanteni sana kwa usikivu wenu Huyu ndiye DC Chonjo ninayemfahamu Kipenzi cha Wana Morogoro ambapo ningetamani aendelee kutumikia Wilaya hii kwa muda mrefu kama itampendeza Mhe. Rais Dkt. John Magufuli ili tuzidi kuiona Morogoro tuitakayo.
Wiki ijayo tutakuwa na Uchambuzi wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. pascala Kihanga.na Makala hizi zinaandaliwa kuwachambua Viongozi wa ngazi za Juu wa Manispaa ya Morogoro.
Post a Comment