BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA MOROGORO YAWATAKA WATAALAM KUTOA MAELEKEZO MAPEMA KABLA YA UJENZI WA MIRADI.
Mstahiki Meya na Mkurugenzi wakiingia ukumbini tayari kwa mkutano. |
Baadhi ya Wakuu wa Idara ya Manispaa ya Morogoro wakiwa katika mkutano huo. |
Baadhi ya Madiwani wakifuatilia mkutano huo. |
Aidha, amewataka Wataalam kufanya kazi kwa pamoja na pale wanapokwama walishirikishe Baraza ili waone jinsi ya kuweza kukwamuana mahala ambapo panaonekana kuna tatizo au panahitaji maelekezo ya kina.
"Niwaombe Wataalam , msiwaone Madiwani wanalalamika na kupiga kelele, hii yote ni kutaka kujua miradi inavyoendelea na kuleta tija kwa wananchi maana hata hizo pesa zinazotumika ni kodi za Wananchi hivyo ni lazima wajue na kufuatilia ili wao wawe mabalozi wazuri wa kuizungumzia miradi hiyo katika vikao vyao na kama tutashirikiana kwa pamoja maendeleo ya Manispaa yetu yatazidi kuwa juu" Amesema Mhe. Kihanga.
Amesema maendeleo ya Manispaa ya Morogoro ni ya wato hivyo Manispaa wakifanya vizuri Mkurugenzi, Baraza la Madiwani , Watumishi, Wakuu wa idara na wananchi wote watasifiwa.
Katika hatua nyengine, akijibu swali la Diwani Viti Maalum Kata ya Kiwanja cha Ndege, Mhe. Dorith Mwamsiku lililouliza mikutano ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi ni endelevu au la muda mfupi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema mikutano hiyo ya hadhara ni endelevu hivyo mpango uliopo ni kushuka Mtaa kwa Mtaa kufuatia agizo la Mhe. Rais la kutaka Manispaa na Wilaya kushuka chini kusikiliza wananchi.
Amesema lengo la ziara hiyo ni kusikiliza na kutatua kero za Wananchi ili kurahisisha huduma kwa jamii pamoja na kufahamu kuhusu miradi mbali mbali inayotekelezwa na kero zilizotatuliwa katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM chini ya Rais wa awamu ya tano, Mhe Dkt John Pombe Magufuli.
Katika kikao hicho pia kulikuwa na maswali ya papo kwa papo ambapo Diwani wa wa kata ya Mji Mpya, Mhe. Wenslaus Kalogeries, amesema katika Soko la Mji mpya kuna mfereji mikubwa imechimbwa lakini haina mwendelezo mzuri pamoja na kuwepo kwa uharibifu wa barabara kipindi kilichonyesha mvua na kutaka kujua changamoto hizo zinatatuliwaje na mamlaka husika.
Kuhusu uendeshaji wa Soko, Sheilla, amesema suala hilo wamekuwa wakilijadili katika vikao lakini wanatarajia kulifikisha katika kwenye kikao cha fedha cha mwezi wa pili cha Baraza la Madiwani kwani wao ndio wenye wananchi na kuona jinsi gani watapanga kwa ajili ya maslahi ya maendeleo ya Manispaa na wananchi kwa ujumla bila kuathiri mambo mengine na kufanya Soko hilo kuwa na tija;.
Akijibu swali hilo, Meneja wa TARURA Manispaa ya Morogoro, Mhandisi James Mnene, ni kweli wakati wa mvua zinanyesha walikusanya taarifa ya barabara zote zilizoharibika na kuzipeleka TARURA Mkoa kwa ajili ya kuweza kupatiwa fedha za dharura ili kuanza matengenezo ya barabara hizo huku akisema suala la mtaro uliochimbwa kupisha barabara yenye urefu wa Mita 670, mtaro huo ulichimbwa kufuatia kukumbwa na changamoto ya maji (water table) lakini walimkata mkandarasi wa barabara hiyo baada ya kuchelewa kushughulikia suala hilo la mitaro jumla ya shilingi milioni 28 na taarifa tangia mwaka jana zilipelekwa TARURA Makao makuu ili kupata fedha hizo lengo likiwa ni kujenga mtaro huo kwa mawe na kuleta ubora.
Katika hatua nyengine, Diwani Kata ya Kihonda, Mhe. Hamisi Kilongo, ameuliza swali la kujengwa kwa majengo mafupi katika Stendi mpya ya Daladala iliyopo Mafiga kufuatia mapendekezo ya kamati ya Fedha, huku Meneja wa TARURA , Eng. James Mnene amesema majengo hayo yalijengwa kwa kuzingatia dizaini na ushauri kutoka kwa Mshauri wa mradi huo na kusema yatakapokamilika jayana shida.
Kwa upande wa Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Eng. Juma Gwisu, amesema Mapaa ya majengo yamezingatiia sababu za eneo husika kutokana eneo la Kijiografia hivyo kama yatabadilishwa yatakuwa na athari zake.
Afisa Ardhi Manispaa Morogoro, Gisbert Msemwa. |
Amesema kwa sasa idara hiyo ina wataalam 11 na wanatakiwa wataalam 72 ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi wa halai ya juu lakini kikubwa ni ushirikianao kwa Madiwani, Wananchi ili kuweza kusaidia katika kukomesha ujenzi holela.
Pia amewataka Viongozi kuanzia ngazi za Mitaa na Kata wanapofanya mikutano na wananchi wawaite na kuiweka agenda ya Ujenzi holela iwepo katika kila mikutanao hiyo ili waweze kuendelea kutoa elimu.
Waandalizi wa mikutano Manispaa ya Morogoro (CMT) , kushoto Afisa Utumishi Manispaa ya Morogoro, Waziri Kombo wakiwa katika mkutano huo. |
Post a Comment