Header Ads

Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro aagiza watumishi wote kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.





Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba.

Gari la Matangazo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi likipita mitaa ya Manispaa ya Morogoro kuhamasisha wakazi wa manispaa hiyo kujitokeza kuandikishwa au kuboresha tarifa zao ifikapo Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaoratajiwa kufanyika tarehe 03  hadi Februari 09, 2020.

MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba,  ameagiza Watumishi wote wa Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro pamoja na Wakuu wa Idara kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais.


Hayo ameyazungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la Wafanyakazi Manispaa ya Morogoro.

Amesema zoezi hilo wasiwaachie Wananchi pekee kwani wao wanatakiwa kuwamfano wa kuigwa na kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi ili wajiandikishe na kutimiza haki zao za Kikatiba.

"Pamoja na kuhamasisha Wananchi kujitokeza  kujiandikisha, nanyie hakikisheni watumishi wote mnajiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura kwani zoezi hili ni muhimu kwa kila mmoja wetu" Amesema Sheilla.

Aidha, pia amewataka Wananchi kujitikeza kwa wingi Kwenda kituoni kuandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura.

Amesema miongoni mwa faidia za kujiandikisha katika uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ni pamoja na Kupunguza malalamiko ya wadau juu ya Daftari la kudumu la wapiga kura, Kuwafanya wapiga kura wajiamini kutokana na taarifa zao kuwa sahihi na salama, Kunapunguza malalamiko ya uchaguzi, Kupunguza vurugu wakati wa uchaguzi, Unajenga usawa na uwazi katika mchakato wa Uchaguzi, pamoja na Kunalifanya zoezi la uchaguzi likubalike.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.