Header Ads

NEMC yawawashia moto Waingizaji na Wazalishaji wa Mifuko mbadala isiyokizi viwango.

Ukaguzi ukiendelea.
Afisa Mazingira Manispaa ya Morogoro, Dauson Jeremia akikagua Soko la Mawenzi. 


WAKATI Serikali ikiwa imepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki ili kuepusha athari za kiafya na mazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na matumizi ya mifuko hiyo, kumeibuka wimbi la matapeli wanaotengeneza mifuko hiyo kinyume na sheria.
Afisa Mazingira Mkoa Morogoro,Venance Segere,(katikati) akikagua mifuko na kamati ya mazingira Soko la Mawenzi Manispaa ya Morogoro.
Utapeli huo umeibuliwa na Baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC)  walipofanya ziara katika Manispaa ya Morogoro na kuwakamata baadhi ya wahusika wanaotengeneza mifuko hiyo na watumiaji pamoja na kampuni za uazlishaji wa vifungashio vya plastiki.
Mifuko ya plastiki iliyokutwa katika kibanda cha  Kiwanja cha ndege.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Afisa Mazingira  Mkoa Morogoro, Venance Segere, amesema kuwa Ofisi ya Mkoa kwa kushirikiana na NEMC wameanza  msako wa kuwabaini waingizaji na wazalishaji wa mifuko mbadala aina ya ‘non woven’ isiyokidhi viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) vya chini ya GSM 70.
Afisa Mazingira Mwandamizi na Mkaguzi wa Mazingira, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Abella Mayungi, (katikati) wakijadiliana jambo katika ukaguzi huo nje ya Soko la Mawenzi.

 Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23, 2020  ambapo amesisitiza kuwa mifuko inayotakiwa lazima iwe na jina la mzalishaji, uzito na mawasiliano ya mzalishaji.

Aidha , amesema  kuwa kumezuka wimbi la mifuko isiyokidhi viwango vilivyowekwa  hivyo matokeo yake wale ambao wameitikia wito wa kufungua viwanda vya mifuko mbadala wanakosa soko.


“Elimu kwa umma itaendelea kutolewa ili watu wajue mifuko ipi hairuhusiwi kutumika na hii itasaidia wazalishaji wa mifuko inayokidhi viwango kupata masoko na kuweza kuisambaza hadi kule kwenye changomoto na bei itakuwa ya kawaida ili kila mtu aweze kununua,lakini zoezi hili ni endelevu kama wenzetu wa NEMC walivyotuelekeza nasisi tutazidi kuzidisha nguvu kuhakikisha tunawatia hatiani wahusika na kupigwa faini kwa majibu wa Sheria” amesema Segere.
Kwa upande wake Afisa Mazingira Mwandamizi na Mkaguzi wa Mazingira, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Abella Mayungi, amesema kuwa zoezi la katazo la mifuko ya plastiki kupitia Kikosi kazi cha Taifa limefanikiwa kwa kiwango kikubwa lakini katika kipindi cha hivi karibuni kuna genge la wahuni limeibuka kuharibu hali ya hewa na kuiletea Taifa sifa mbaya katika mifuko mbadala.
Fomu ya faini.

Mayungi amesema  kuwa kuanza sasa vifungashio vya plastiki vya katoni za maji havitaruhusiwa na kuwa badala yake yatumike maboksi kwani yanaweza kurejelezwa hivyo ni rafiki wa mazingir huku akiongeza kuwa magazeti hayaruhusiwi kufungashia bidhaa zikiwemo vyakula kama nyama kwani ni hatari kwa afya zikiwemo magonjwa ya kansa.

Naye Afisa Mazingira Manispaa ya Morogoro, Dauson Jeremia, amesema kwa sasa mifuko hiyo imeondolewa lakini bado kuna changamoto ya vifungashio kugeuzwa vibebeo huku akionya viwanda vya vinavyojihusisha na uzalishaji wake.

“TBS imeshatoa kanuni za namna gani mifuko mbadala inayozalishwa lakini bado tunaona mifuko hii inazalishwa kwa wingi na tunajua bayana lazima mifuko hii iwe na GSM 70 ili kuwalinda lakini wale tunaowalinda wanazalisha usiku wanapeleleka sokoni sasa Serikali haijalala tumeanza msako wa kuwabaini na tutawachukulia hatua,licha ya hapo pia tumejitahidi kuwaelimisha na kutoa elimu pana juu ya mifuko mbadala na kufuata taratibu za kwenda TBS ” amesema Jeremia.

Aidha amesema  kuwa tayari kikosi kazi hicho kimekamata kiwanda kinachozalisha mifuko hiyo kilichopo Manispaa ya Morogoro cha MZ  Packaging Industry, Morogoro Plastic, Kweba plastic Industry kilichopo nane nane na kupiga faini ya Milioni 20 Kiwanda cha MZ Packaging kutokana na kuwakuta wakiendelea kuzalisha na maduka mengine yamepigwa faini ya shilingi 30000 baada ya kukutwa na mifuko ya plstiki na viwanda vidogo vya mifuko mbadala  wahusika walikubali na kupigwa faini ya shilingi laki mmoja na kupiga marufuku kuendelea na uzalishaji huo  huku akitoa rai kwa wananchi kutoa taarifa pindi wanapoona viwanda kama hivyo.

Zoezi hilo la   msako wa kuwabaini waingizaji na wazalishaji wa mifuko mbadala aina ya ‘non woven’ isiyokidhi viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) vya chini ya GSM 70 lilianza Januari 20, 2020.

Miongoni mwa maeneo waliyotembelea leo katika msako huo ni pamoja na Soko la Mawenzi, Soko la Chamwino pamoja na Kata ya Kiwanja cha Ndege.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.