Mkurugenzi Manispaa Morogoro kuanza ziara kesho ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, kesho anatarajia kuanza ziara ya kutatua kero za Wananchi kuanzia ngazi za Kata ili kurahisisha huduma.
Katika ziara hizo, amesema ataambatana na timu ya Wataalamu kutoka TANESCO, MORUWASA, PSSSF,TARURA, NIDA, TANROAD , UHAMIAJI, na wengine.
Miongoni mwa kero zitakazo sikilizwa ni pamoja na kero ya Migogoro ya ardhi, afya, huduma za umeme, mazingira, elimu, n.k.
Pia ataambatana na Wakuu wa Idara mbali mbali watakao pokea na kujibu kero hizo.
Amesema hataki kuona tena Kero hazitatuliwi katika ngazi za chini ambapo zinaweza kusikizwa na Mtendaji wa mtaa, Mwenyekiti wa mtaa, Mtendaji kata,au Afisa Tarafa.
"Ofisi yangu imekuwa ikipokea wananchi wanaowasilisha Kero zao katika Ofisi yangu, Sasa Kero hizo zinakuwa hazipatiwi ufumbuzi na badala yake wananchi wanakimbilia kwa Mkuu wa Wilaya au wanasubiri Mkuu wa Wilaya awatembelee ili waeleze Kero zao jambo hili halikubaliki"Amesema Sheilla.
Post a Comment