Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro ataka zooezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura liendeshwe kwa kuzingatia sheria na kanuni za TUME.
Maafisa Wasaidizi waandikishaji ngazi ya Kata wakila kiapo. |
|
Ameyazungumza hayo, wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Maafisa Waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata katika ukumbi wa Manispaa ya Morogoro leo Januari 27,2020.
Kamishina wa Tume ya Uchaguzi, Marry Longway (Jaji Mstaafu). |
Akizungumza na Waandishi wa habari, amewapongeza washiriki wote walioteuliwa na Tume kuendesha na kusimamia zoezi hilo muhimu la Uandikishaji wa Wapiga kura.
Baadhi ya Maafisa wandikishaji wasaidizi wakila viapo leo. |
Baadhi ya Maafisa wandikishaji wasaidizi wakijaza viapo leo. |
I.T Manispaa ya Morogoro wakiteta jambo. |
Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Mjini Manispaa ya Morogoro, Gaudiosa Mbwana (katikati) ,akisoma viapo (kushoto)Afisa Uandikishaji Manispaa ya Morogoro, Pendo Chagu. |
Pia amewaambia kwamba Mawakala wa Vyama vya Siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura na watazamaji watazamaji wakati wa zoezi zima la uboreshaji ambao watapatiwa vibali maalum ambavyo vitawaruhusu kuingia katika vituo vya kuandikisha jambo ambalo ni muhimu na litasaidia kuleta uwazi katika zoezi hilo.
"Lazima mtambue kwamba , Mawakala wa Vyama Vya Siasana Watazamaji hawatakiwi kuwaingilia watendaji mnapotekeleza wajibu wenu, hivyo maelekezo zaidi kuhusu suala hili yapo kwenye vitabu vya maelekezo mlivyopatiwa na ni muhimu kuyazingatia ili zoezi letu lifanyike kwa mujibu wa Sheria , kanuni na maelekezo" Ameongeza Sheilla.
Mbali na melekezo, amewaambia kuteuliwa kwao kumetokana na kuaminiwa hivyo wanauwezo wa kufanya kazi hiyo, kikubwa ni kujiamini na kujitambua na kufuata maelekezo yatakayotolewa na Tume ili waweze kufanya kazi wakati wa zoezi la Uandikishaji pamoja na kufuata Sheria , kanuni, maelekezo na miongozo.
Amesema Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, imedhamiria kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi mkubwa na kuwataka watendaji kuhakikisha wanayajua na kuyatambua vyema maeneo watakayofanyia kazi ikiwemo miundombinu ya kufikia katika Kata na Vituo.
Hata hivyo, amesema katika kufanikisha zoezi hilo, kunahitajika ushirikianao mkubwa kati ya watendaji wote , Serikali , Vyma Vya Siasa na wadau wengine wote, pia waongeze ushirikiano mzuri wa karibu na Ofisi ya Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Morogoro wakati wote watakapokuwa wanahitaji ufafanuzi au maelekezo katika kazi zao huku akiwatakia kazi njema katika mafunzo yao.
Kwa upande wa Kamishina wa Tume ya Uchaguzi, Marry Longway (Jaji Mstaafu) , amewataka Waandikishaji kuzingatia muda wakazi kabla ya saa 2:00 asubuhi wawe washafika katika vituo ili ifikapo saa 2:00 asubuhi kazi zianze kufanyika ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi na kuendelea katika kazi nyengine za uzalishaji.
"Lazima ufike mapema, uangalie BVR Kit imefungwa, fomu zako zipo tayari , kalamu yako inaandika vizuri, sio inafika saa 2:00 asubuhi wewe ndio unafika unajisachi mfuko peni haiandiki fomu hazionekani , BVR haijawashwa sio utaratibu lakini najua saa 12 jioni ndio muda wa kufunga kazi lakini lazima uangalie taarifa zako umezipangaje kwahiyo mkifuata hatua zote zoezi letu litakwenda vizuri bila matatizo na wananchi, mawakala wa Vyama Vya Siasa wala watazamaji" Amesema Longway.
Pia amewataka waandikishaji kuhakikisha wanawaandika majina na kuanza nao siku inayofuata kwa wale ambao muda wa kufunga kazi utawakauta wakiwa katika foleni ili kukwepa migongano na migogoro kwa wananchi.
Amesema vipaumbele vitolewa kwa Watu wazima, (Wazee), Watu wenye ulemavu, Wajawazito pamoja na wagonjwa hawaruhusiwi kukaa foleni.
Naye, Afisa wa Jimbo la uchaguzi la Morogoro, Waziri Kombo, amewapongeza maafisa hao kwa kuaminiwa na kuchaguliwa kuifanya kazi kubwa ya kitaifa ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura.
Aidha amewataka maofisa hao kuwa wasikivu na kuzingatia mafunzo watakayopewa kuhusiana na uendeshaji wa zoezi hilo.
Hata hivyo Kombo amesema hawatamvumilia mtu yoyote atakayekuwa mzembe wakati wa uboreshaji wa Daftari.
" Kama Manispaa yetu ya Morogoro tunataka tuwe watu wa kwanza kitaifa kuandikisha watu wengi zaidi na hii inawezekana tukiwa na weledi na tukizingatia mafunzo tutakayopewa" Amesema Kombo.
Zoezi la uboreshaji Daftari la kudumu la mpiga kura katika Mkoa wa Morogoro linatarajiwa kuanza katika Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro, Halmshauri ya Mji wa Ifakara, Halmshauri za Wilaya ya Gairo, Kilombero, Kilosa, Morogoro na Mvomero kuanzia tarehe 03 hadi 09 Februari 2020.
Post a Comment