DC Chonjo azindua Mapipa 50 ya taka yenye thamani ya shilingi Milioni 591 Manispaa ya Morogoro.
MKUU a Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, amezindua mapipa ya kuhifadhia takataka(skipbacket) 50 yenye thamani ya Tsh 591,519,500 ambapo kwa leo jumla ya mapipa 35 yenye thamani ya Tsh 414,063,650.00 ameya pokea ikiwa ni awamu ya kwanza ambapo Manispaa ya Morogoro ilitenga jumla ya Tsh 591,519,500 kwaajili ya ununuzi wa mapipa 50.
Mapipa ya taka. |
Zoezi hilo limefanyika leo Januari 18, 2020, katika Viwanja vya Kata ya Mji Mkuu, ambapo amewataka wanachi kuvitumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Gari aina ya Skip Loader ikinyanyua Pipa la taka |
Mkuu wa Wilaya (katikati) akipitia taarifa ya Mapipa ya taka . |
Amesema Mapipa hayo yametumia jumla ya Shilingi Milioni 591 kila pipa likiwa na thamani ya shilingi milioni 11 na kusababisha mapipa kuwa na mapipa 65 huku mapipa 35 yakiwa yamezinduluiwa leo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe. Pascal Kihanga. |
Äidha, amesema Mapipa hayo yatagawanywa katika Masoko, maeneo yenye msongamano wa watu, maeneo yenye shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii.
Mara baada ya Mapipa hayo kujaa taka yatakuwa yanabebwa na gari tatu za Manispaa aina ya 'Skip Loader' ambapo Manispaa imeagiza magari mengine 2 ya aina hiyo kwa ajili ya uondoaji wa mapipa ya taka.
"Mapipa haya yataboresha usafi wa mji kwani wananchi watakuwa na sehemu ya kuwekea /kuhifadhi taka zao kwa muda badala ya kuzitupa hovyo au kuziweka kando kando ya barabara, niwaombe wananchi tuendelee kulipa ada ya taka ya kila mwezi ili kuwezesha Kampuni / Vikundi vya usafi na Manispaa Manispaa yetu kuendelea kutoa huduma bora kwa Wananchi" Amesema DC Chonjo.
Amesema Morogoro ipo kati kati ya Mji Mkuu wa Makao Makuu ya Serikali Dodoma pamoja na Mji Mkuu wa Biashara Dar Es Salaam, hivyo ili Morogoro iwe Jiji kuna vigezo mmbalimbali ikiwemo suala la Usafi, mandhari husika hivyo kuna haja ya kuwa wasafi.
Pia amewataka Madiwani wa Manispaa ya Morogoro kuhimiza na kusimamia usafi katika kata zao kwa kuwa wao ndio wenyeviti wa Kamati za Maendeleo ya Kata.
" Mimi nilivyofika hapa Morogoro mwaka 2016 nilikuta kambi ya kipindupindu iliyodumu kwa miaka 5, kuanzia mwezi wa 11 , 2016 kipindupindu kilikuwa ni historia kwa manispaa yetu ya Morogoro, hiyo nayo ni sababu iliyotufanya tuchelewe kuwa Jiji, navitaka vikundi vya taka viwajibike kuanzia ngazi za Mitaa na Kata na kama vitashindwa kufanya vizuri vitafutwe vyene uwezo wa kutatua kero za taka ambapo amesema sio vyema maafisa mazingira kufika katika mitaa yote 294 " Ameongeza DC Chonjo.
Katika hatua nyengine, ameutaka Uongozi wa Soko la Manzese kusimamia uasfi na mazingira kwani soko hilo hariridhishi.
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogro, Sheilla Lukuba, amesema fedha za kununulia mapipa ya kuhifadhia taka ngumu wamenunua kupitia fedha za kimkakati ambazo walipatiwa na Mhe. Rais Dkt. John Magufuli.
Amewataka wananchi kutpotupa taka pembeni badala yake wazihifadhi taka hizo katika vyombo husika na wale watakao kaidi watapigwa faini kwa mujibu wa sheria za mazingira.
Mbali na uzinduzi wa mapipa hayo amesema pia suala la usafi liwe katika damu na sio wananchi wangoje hadi viongozi wafike ndipo wafanye usafi.
" Suala la usafi ni kama unavyooga kila siku, jinsi ya kupiga mswaki bila kusimamiwa, kwahiyo niwasihi wanqanchi wa Manispaa ya Morogoro naomba tufanye usafi bila kushurutishwa , kwani hata Mhe. Rais Dkt John Magufuli amewaonesha Watanzania kwa kliona na kulipa kipaumbele suala la usafi" Amesema Sheilla .
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amesema ujio wa Mapipa ya takataka uendane na usafi wa mazingira.
Mbali na hapo, amesema kuwa sula la usafi katika Soko la Manzese bado ni changamoto na hariridhishi hali iliyomfanya Mkuu wa Wilaya kuwa mkali sana.
Amesema kuwa asilimia kubwa ya wafanyabiashara wanafanya usafi katika sura ya nje lakini katika vizimba vyao kwa chini kumekuwa kuchafu sana jambo ambalo halipendezi na linatakiwa kuchukuliwa hatua ili soko hilo liwe safi.
Amewaomba wafanyabiashara wa Masoko yote yaliyo katika Manispaa ya Morogoro wajitahidi kufanya usafi.
"Tunaweza kuwa na vyombo vizuri vya usafi tukashindwa kufanya kazi zenyewe, amesema kazi hiyo iendelee kufanyika hivyo lakini pia amemuomba Mkurugenzi kufuatilia hayo magari yaliyobakia yaweze kuja mara moja kwa ajili ya kuwasaidia wananchi " Amesema Mhe. Kihanga.
Post a Comment