Header Ads

Mkurugenzi Manispaa Morogoro ageuka mbogo suala la uchelewaji Kazini.





Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akizunguma na Diwani Kata ya Mafisa(katikati) Mhe. Daud Salumu leo alipotembele Kata hiyo kuangalia nidhamu ya kujali muda kazini, (kulia) afisa Mazingira Samwel Subi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, alipokuwa katika ziara fupi ya kufuatilia suala la nidhamu kazini ya kujali muda wa kuwahi kazini kwa Watendaji na Watumishi katika Kata leo Januari 13, 2020.

Mkurugenzi akisaini kitabu cha mahudhurio Kaya ya Kingo leo

Akizungumza hayo mapema , amesema bado wapo watumishi katika ngazi za Kata na Mitaa wamekuwa na nidhamu mbovu ya kuchelewa kazini jambo ambalo limekuwa sugu huku akiwataka watumishi kubadilika na kuendana na kasi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. John Pombe Magufuli ya hapa kazi tu.


"Mpo hapa kwa ajili ya kumsaidia Mhe. Rais , Dkt. John Magufuli, hivyo wafanyakazi mnawajibu wa kuwahi kazini saa 1:30 asubuhi kama ilivyopangwa kwa mujibu wa taratibu za Utumishi wa Umma na kutoka saa 9:30 Mchana baada ya muda wa kazi, hatuwezi kuendelea kuvumilia tabia ya watu kuendelea kumwibia Mwajiri muda wa kufanya kazi, sisi na timu yangu tumewahi kazini na tunachelewa kutoka helewa hizi kazi tusiwaachie wanafunzi wa Field, lazima wahusika muwahi ili muwapatie maelekezo ya kina na tambueni hawa sio waajiriwa wanajitolea muda wao ukimalizika wanaondoka " Amesema Sheilla.

Aidha amesema kitendo cha kuchora mstari kwa wino mwekundi ni kuashiria kwamba wale waote watakao kuja mwisho wa wino watahitajika Katika Ofisi ya Utumishi kwa ajili ya kupatiwa barua zao za utovu wa nidahmu za kuchelewa kufika kazini bila taarifa ya msingi huku huduma kwa wananchi zikichelewa na kuchelewesha maendeleo.


"Leo nimeona nifanye ziara hii fupi ya kushtukiza kwa kupitia katika Kata zangu ili kuangalia mahudhurio ya watendaji, lakini nilichobaini bado kuna hali ya nidhamu mbovu ya kuchelewa kazini, katika tembea yangu Kata ya Mafisa nimemkuta Mtendaji wa Mtaa tu na wanafunzi wa Field, na  Kata ya Kingo nimemkuta muhudumu tu sijafurahishwa na hali hii, huku ni kuwaibia Wananchi pesa zao , wanyonge wamekuwa wakilipa

kodi na nyie mnapewa misharahara hamuitumii ipasavyo maana usipokuja na ukija bado mishahara yenu upo pale pale , tubadilike tufanye kazi na mishahara yetu ni nguvu za wanyonge amabo tuna wajibu wa kuwatimizia kero zao na kutoa huduma nzuri bila ya upendeleo" Ameongeza Sheilla.

Hata hivyo, amesema kuwahi kazini kuna kwenda na kuanza kazi muda huo huo sio mtu anawahi kazini kisha anaazna kusoma magazeti au kupiga soga kwa hili hata weza kulifumbia macho na atawachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria kwa wale wenye tabia kama hizo.

Amesema katika Manispaa yake anataka kazi zifanyike na kama yupo mtumishi au mtendaji anaona hawezi kuendana na kasi yake atafute mahala pengine kwa kufanyia kazi na sio katika Manispaa ya Morogoro.

Katika hatua nyengine, amewataka wale wote ambao wamechelewa kufika kazini katika Kata alizotembelea wafike katika Ofisi ya Afisa Utumishi Manispaa ili wapatiwe barua zao kutokana na kuchelewa kazini.

Mbali na Watendaji  wa Kata na Mitaa pia amewataka watumishi wa Manispaa kuzingatia muda wa kuingia kazini na kuwatumikia wananchi ili kero zote zilizopo mitaa zipungue na kuepusha mabango yanayoandaliwa na Wananchi kufuatia ujio wa Viongozi wa Juu wa Nchi wanapofanya ziara.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.