Header Ads

Manispaa ya Morogoro yaahidi kuendeleza ushirikiano na Wamachinga , ikiwataka kufuata sheria katika maeneo yao ya biashara.




KAIMU Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim, amesema Manispaa ya Morogoro itazidi kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa na Wamachinga kwa kutambua umuhimu wa kundi hilo muhimu.


Hayo ameyasema leo Januari 11, 2020 katika mkutano wa Wamachinga wakujadili maendeleo yao na mipango wakati wa kumwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa aliyepata udhuru kwa kutekeleza majukumu mengine.

Amesema suala la wamachinga zamani walikuwa hawapewi ushirikiano walikuwa ni watu wa kubughuziwa na kuhamishwa hamishwa lakini Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli imewatendea haki wamachinga na kuwaona ni kundi  muhimu katika kuelekea Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa Kati.

Amesema ushirikiano na wamachinga haukuanza leo tu bali upande wa manispaa walikuwa wakishirikiana vyema katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa manispaa katika vikao hata hivi karibuni katika mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi uliitishwa na Mkurugenzi walishiriki.

"Tunatambua mchango wenu, tumeshirikiana katika kazi mbali mbali ikiwamo ya mwenge uchangiaji wa madawati, kwahiyo hata ukiangalia kwa upande wa manispaa yetu yapo maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya shughuli zenu  za biashara ikiwamo masoko na minada ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais baada ya kuwatambua rasmi kundi hili na kuwataka mfanye biashara zenu  popote pale bila kuvunja sheria kwa kuwapatia vitambulisho rasmi vya kuwatambua pamoja na wajasiriamali wengine" Amesema Chamzhim.

Amesema katika ushirikiano huo na jinsi wamachinga walivyojipanga imesababisha hadi watu kutoka Mikoa mingine wanakuja Manispaa ya morogoro kwa ajili ya kujifunza kwani kabla ya Mhe. Rais kutoa vitambulisho vya wajasiriamali wao tayari walishakuwa na mfumo wao wa vitambulisho.

Kwa upande wa manispaa wamefurahishwa  sana kuona umoja huo ulivyo imara mna kujitengenezea sheria , kanuni na taratibu na maelekezo ya kuonyana pale mmoja wapo anakwenda kinyume na malengo ambapo wameahidi kuendeleza ushirikiano huo pale wanapoona kuna tatizo Ofisi ya Mkurugenzi ipo wazi watapatiwa majawabu na kupewa ushirikiano mkubwa wa kupeleka mbele gurudumu la maendeleo kwa wamachinga pamoja na maendeleo ya wananchi waishio Manispaa ya Morogoro.

Hata hivyo amewataka kutoa taarifa yoyote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani kwani wao wapo kwa ajili ya Usalama na Ulizni wa wananchi wao sio kuona baadhi ya wananchi wanaumizwa na watu wachahce kwa ajili ya maslahi yao binafsi na endapo watu hao watakuwepo watawachukulia hatua kali za kisheria.

Hata hivyo Diwani Kata ya Sultan Area, Mhe.Peter Dhahabu,  amesema katika kipindi hiki cha karibuni, wameshuhudia mabadiliko makubwa sana hususani katika miradi inayotekelezwa katika Manispaa hiyo ikiwamo miradi mikubwa ya kimkakati kama vile mradi wa Soko Kuu la kisasa lililopo Kata ya Mji Mkuu pamoja na Mradi wa Stendi Mpya.

Amesema kuwepo na miradi mikubwa ndani ya Manispaa kutasaidia kuingizia Manispaa pato la ndani na kuacha kutegemea fedha za Ruzuku kutoka Serikali kuu.

Pia amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, kwa kuwa karibu na Wamachinga katika  kuwashirikisha  kwa kila jambo kitu ambacho kinawajengea faraja Wafanyabiashara na kuona Serikali inawaunga mkono kama alivyotamka Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwataka Wamachinga kufanya biashara zao bila ya kubugudhiwa.

Naye Mwenyekiti wa Wamachinga Manispaa ya Morogoro,  Faustine Almas , ameupongeza Uongozi wa Halmshauri ya Morogoro chini ya Mstahiki meya, Mkurugenzi na wakuu wa idara pamoja ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya  Morogoro, Mhe. Regina Chonjo kwa ushirikiano mzuri wanaoutoa na kuwafanya kuwa kitu kimoja kwa kuwatengea maeneo ya kufanyiabishara bila kunyanyasika.

Mbali na hayo, amesema Manispaa ya morogoro imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati wao kama wamachinga wanaungana na Manispaa kuwaombea ili wazidi kuendelea kuanzisha miradi mipya kwa maendeleo ya wananchi wa Manisnpaa ya Morogoro.

Amesema kwa sasa wapo katika zoezi la usajili  wanachama katika jumuiya yao mpaka sasa jumla ya wanachama 260 wameshaandikishwa huku wakiwaomba wamachinga waendelee kujitokeza katika Ofisi zao wapatiwe usajili na kutekeleza sheria.

Miongoni mwa changamoto alizozitaja Mwenyekiti wa wamachinga, ni pamoja kutengewa eneo moja la kufanyia biashara kama Machinga Complex kwani wengine  hawana uwezo wa kukodisha  makubwa  ya mjini,  suala la ulinzi na usalama jambo ambalo bado linatika sana mashaka kwani ulinzi katika maeneo yao ya biashara ni dhaifu na hawapati ushirikiano katika hilo na kupelekea baadhi ya wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa wasiwasi licha ya uongozi wa manispaa upo hivyo wameomba suala hilo litazwame kwa jicho la tatu.

Aidha amesema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kuchangisha michango wanapopatwa na misiba au mtu kuumwa kinyume na taratibu jambo amablo amelipiga marufuku na kuwataka wafanyabisahra wanaopatwa na misiba au wagonjwa  kabla hawajachagisha wafuate utaratibu katika Ofisi zao ili waweze kupewa kibali cha kuchangisha kuliko kujichangishia kiholela jambo lianloleta usumbufu na kutokuwa na imani na viongozi wa jumuiya hiyo na wale wanaochangisha.

"Niwaombe ndugu zangu mwaka 2020 tubadilike hatutamuonea haya mtu yeyote atakayepita na daftari kuchangisha michango amabpo Ofisi haimtambui, tutamchukia hatua kali na kumfikisha Mahakamani,amesema umoja huo una mwansheria hivyo gharama zote mtu alizochangisha atazilipa kuanzia alivyoanza hadi alipoishia "Almas

Pia wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, kwa kuwa karibu nao na kuwashirikisha  kwa kila jambo kitu ambacho kinawajengea faraja Wafanyabiashara na kuona Serikali inawaunga mkono kama alivyotamka Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwataka Wamachinga kufanya biashara zao bila ya kubugudhiwa.

Pia wamemshukuru Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapatia kibali cha kufanya biashara zao pembezoni mwa barabara na kando kando ya mitaa kwani awali waliishi maisha ya kutanga tanga ya  kunyang'anywa bidhaa zao lakini Mhe. Rais ameliona hilo na kuwaondoa  kwenye mateso.

Hata hivyo, amewaomba Wafanyabisahara wenzake kuwa ruhusa ya kibali cha wao kupanga biashara zao barbarani sio wakiuke shereia ,wanatakiwa kuzingatia sheria na kuhakikisha mara baada ya kufanya biashara zao wasogeze meza pembeni ili kuruhusu maeneo hayo yaweze kutumika kwa matumizi mengine.

Kwa upande wa Mweneyekiti wa Magulio Mkoa wa Dar Es Salaam,  Ndg. Mrisho Issa, amesema wafanyabiashara wa magulio wamekuwa wakitozwa ushuru barabarani jambo ambalo anataka ufafanuzi wa hilo ili kuangalia maelekezo aliyoyatoa Mhe. Rais ni hayo au hao wanaowatoza ushuru wanakwenda kinyume na agizo la Mhe. Rais.

Pia amesema suala la nidhamu kwa baadhi ya wafanyabishara hairidhishi kwani Serikali licha ya kuwapatia maelekezo lakini wamekuwa wakwanza kukiuka na kwenda kinyume na wakati unawaelekeza wamekuwa wakwanza kurusha ngumi na kujichukulia sheria mkononi, amewaomba waache tabia hiyo mara moja kwani Serikali yao inawapenda na kuwathamni sana na kutambua kundi hilo kama moja ya makundi muhimu ya uzalishaji mali kwa Taifa hili.

Amesema kama wamachinga wakiweka nidhamu mbele na kuzingatia maagizo ya viongozi basi wataendelea kupata fursa zaidi tofauti na hii ya kufanya biashara kwa uhuru bila kusumbuliwa.







No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.