Header Ads

Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro afanya ziara ya kutembelea ukarabati wa madarasa Shule za Sekondari Lupanga, Kayenzi na Kihonda leo Januari 2,2020.



Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba (katikati), kutoka kushoto Mhandisi Manispaa ya Morogoro, Eng. Juma Gwisu pamoja na Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Morogoro, Dkt. Janeth Barongo.

Amesema lengo la kutembelea ujenzi wa ukarabati wa madara ni kuongeza kasi ya ujenzi ili kuhakikisha madarasa yote yaliyo katika shule tajwa yanakamilika  kwa wakati ili wanafunzi wote waliofaulu kwenda kidato cha kwanza mwaka 2020,  wanasoma na hakuna mwanafunzi atakayebakia nyumbani.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Kayenzi, Chuma Sechondi, amesema mwaka huu wamepokea wanafunzi 600 hivyo wote watasoma kwakuwa wanavyumba vya mdarasa ya kutosha.

Ameushukuru Uongozi wa Manispaa kwa kwakamilishia Jengo la utawala huku akisema vyumba 3 vilivyokuwa vikitumika na Waalimu kama Ofisi wanavigeuza kuwa madarasa ya kusomea.

Amesema licha ya kuwa na madaras ya kutosha lakini wanakabiliwa na changamoto ya Viti na meza hivyo kufuatia vikao walivyokaa na wazazi walikubaliana wasaidiane japo sio wazazi wote walioonesha utayari katika jambo hilo.






















No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.