Header Ads

Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro atembelea Kituo cha afya Mafiga kukagua suala la uchelewaji kazini.


Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba , akimbeba mtoto wakati wa kukagua kituo cha Afya cha Mafiga kilichopo Hlmashauri ya Manispaa ya Morogoro leo Januari 27/2020.

Amemuagiza Mganga wa Kituo cha Afya cha Mafiga, kuhakikisha wale waliochelewa kazini baada ya saa 7:30 asubuhi majina yao yawasilishwe katika Ofisi ya Afisa Utumishi Manispaa ya Morogoro.
Amesema muda wa kufika kazini ni saa 7:30 na kutoka ni saa 9:30 mchana hivyo kuchelewa kuingia kazini na kuwahi kutoka ni kumuibia mwajiri muda wa kazi na mshahara .

Mbali na hapo alipata nafasi ya kutembelea Wodi ya Wazazi na kuona maendeleo ya Kituo hicho cha afya kinavyotoa huduma bora kwa Wananchi.

Pia amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi hususani wakina Mama kwa ajili ya kupima Saratani ya Shingo ya Kizazi.

Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akisaini katika kitabu cha wageni alipowasili katika Kituo cha Afya Mafiga kwa ajili ya kuangalia nidhamu za kuwahi kazini.

Magari ya kubebea wagonjwa , (ambulance) yakiwa katika utaratibu wa kutengezwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ili yaendelee kutumika kwa Wananchi. 

Mkurugenzi Manispaa Morogoro, Sheilla Lukuba, akimsalimia mmoja wa wagonjwa katika Kituo cha Afya Mafiga.








































No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.