Header Ads

KIPIRA AWATAKA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM KUONDOA TOFAUTI ZAO



MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Salum Kipira, amewataka,  wanachama wa jumuiya hiyo, kuondosha tofauti walizokuwa nazo kabla ya uchaguzi ili kuona jumuiya inaendelea kufanya kazi za chama sambamba na kuhakikisha CCM inaendeleza ushindi wa kishindo katika Chaguzi zote za usoni.

Kauli hiyo ameitoa Julai 15/2023 katika Kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, kwenye Ukumbi wa Kingo Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro.

Kipira, amesema kuwa ili jumuiya iweze kuendelea kufanya kazi ni vyema ushirikiano uimarike ili kuweza kufanya kazi.

Aidha, amesema kuwa  uchaguzi umekwisha kilichobakia ni kuvunja Makundi na kuendelea kufanya kazi za Chama kwa Ushirikiano wa hali ya juu kama hapo awali.


"Mimi Sina budi nawashukuru sana wanachama wenzangu kwa kuniamini na kuniona nafaa kuongoza nafasi hii katika kipindi cha pili , naahidi kukulipeni kwani mumenionesha imani na nitakulipeni Imani kwani nilishinda kwa kishindo, kilichobaki kuvunja Makundi, awamu hii mimi ni Kipira wa tofauti sana, Timu yangu ya Utekelezaji ipo vizuri na kamati zangu za Wilaya, hakuna maneno tena sasa ni kazi ili kukisaidia  chama chetu cha CCM na Serikali yake chini ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ,"Amesema Kipira.

Hivyo, amewataka  viongozi na wanachama wa Jumuiya ya wazazi kumpa ushirikiano katika utendaji wake wa kazi ili kuona jumuiya hiyo inaendelea kwenda vizuri katika kufanya kazi zake.


Ameshukuru  Chama cha CCM kwa kumteua kugombea nafasi hiyo, na kuahidi kuendelea kufanya kazi nao kwa karibu na kuona wanashinda kupitia chaguzi mbalimbali, zikiwemo chaguzi za Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025.


Sambamba na hayo, ameahidi  kuwa jumuiya yao itakuwa ya mfano na kuendelea kushirikiana na chama ili kuona wanakivusha hasa katika chaguzi mbalimbali zitakazofanyika 2024/2025.


Amesema  atahakikisha wanafikia Malengo katika Sera yao ya Elimu, Malezi na Mazingira.


Pamoja na hayo, amesema baada ya Baraza hilo Jumuiya imepanga mikakati ya kuona mipango yao kazi yanakwenda kama ilivyokuwa ikiwemo kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ili Jumuiya iweze kujiendesha yenyewe na kujitegemea.


Pi, amewataka  wanachama hao kuacha majungu kwani hayasaidii katika utendaji wa kazi hasa za siasa kwani jumiya hiyo iweze kuwa mfano katika Chama.


Upande wa wanachama wa jumuiya hiyo wameahidi  kumpa ushirikiano ili kuona jumuiya hiyo inakwenda vizuri.


Hata hivyo,  amewashukuru Taasisi ya EGG Tanzania chini ya Mkurugenzi wake , Jumanne Mpinga kwa kusaiodia sekta ya elimu hususani katika uchimbaji wa Visima shuleni.


Mwisho,amempongeza Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Morogoro, Gabriel Paul ,kwa ushirikiano wake anaoutoa katika Jumuiya hiyo pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela ,kwa kazi kubwa ya kutekeleza miradi ya Maendeleo katika kutimiza ndoto ya Manispaa kuwa Jiji.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media

SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL: chombo huru media.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.