DC NSEMWA AWATAKA WATENDAJI KUONGEZA KASI YA UTOAJI ELIMU YA HUDUMA YA LISHE KWA WANANCHI.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Rebeca Sanga,amewataka Watendaji wa Kata, Mitaa kwenda kuiweka LISHE kuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao na mikutano yao yote.
DC Nsemwa, amesema ili kuhakikisha kuwa Wilaya ya Morogoro inaondokana kabisa na matatizo yote yatokanayo na ukosefu wa LISHE likiwamo tatizo la UDUMAVU ni lazima sasa Watendaji waongeze juhudi katika kuelimisha umma juu ya madhara yatokano na kutozingatia kanuni za lishe na kwamba njia pekee iliyopo ni kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha kwa kushirikiana na wataalamu wa Lishe kutoka katika Halmashauri.
Adha ,amesema lengo la Serikali kuja na mpango wa utekelezaji wa afua za lishe ni kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya udumavu na utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano.
"Niwatake sasa Watendaji wote kwenda kutoa elimu ya kutosha kwa kushirikiana na wataalamu wa Lishe, mkatoe elimu hiyo katika kikao na mikutano yenu yote na kwamba suala la Lishe liwe ni ajenda ya kudumu kwenu, niendelee kuwakumbusha Watendaji wote kwenda kusimamia suala la utoaji wa chakula mashuleni suala ambalo ni utekelezaji wa maahizo ya Serikali kuu," Amesema DC Nsemwa.
Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Dr. Charles Mkumbachepa, amesema kuwa Manispaa inaendelea na juhudi za utekelezaji wa shughuli za Lishe kama ambavyo takwa la Serikali na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kinavyowaelekeza ili kwenda kuondoa kabisa tatizo kubwa la udumavu kwa watoto.
Kuhusu huduma ya chakula shuleni, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya ,Morogoro, Gabriel Paul, amesema shule 27 zinatoa huduma ya chakula shuleni na shule 2 zimeshindwa kutoa huduma hiyo kutokana na wazazi kushindwa makubaliano ya uchangiaji chakula.
Gabriel, amesema kuwa ameomba kuwa na azimio la pamoja la wazazi kuwekewa sheria ambayo itawabana moja kwa moja katika kulipia gharama za chakula shuleni kutokana na makubaliano yao.
Kwa upande wa Afisa Lishe Manispaa ya Morogoro , Jackline Mashurano ,amesema katika kupunguza udumavu kwa watoto wameendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa lishe kutekeleza afua zinazoleta matokeo makubwa katika siku 1000 za kwanza za maisha ya mtoto.
Mwakilishi wa mradi wa USAID Lishe endelevu, uliokuwa ukifadhiliwa na Shirika la SAVE THE CHILDREN INTERNATIONAL MOROGORO , Elina kweka, amesema kuwa mradi huo umeisha muda wake kwani umekuwa na mafanikio makubwa tangia kuanzishwa kwake mwaka 2018-2023.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia, bila ya kuingia website
Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru_media
SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL: chombo huru media.
Post a Comment