Header Ads

DIWANI TUNDA AKABIDHI MATOFALI 1000 UJENZI WA VYOO SHULE ZA MSINGI MWERE

DIWANI wa Kata ya Kingo Manispaa ya Morogoro , Mhe. Amini Tunda, amekabidhi msaada wa Matofali 1000 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo Shule za Msingi Mwere A na B.

Msaada huo ameutoa Julai 17/2023 katika ziara ya Kamati za Huduma za uchumi, Elimu  na Afya ambayo yeye ndiye mwenyekiti wa Kamati hiyo.

Mhe. Tunda, amesema  kwamba anatambua kwamba ana wajibu wa kuhakikisha

afya za vijana wanaosoma katika shule hizo  zinakuwa salama hivyo ametoa kama kiongozi na mzazi wa watoto hao.

"Nimetoa msaada huu kama Diwani wa Kata hii kutokana na kuguswa kwangu kutokana na changamoto nyingi zinazowakabili wanafunzi na Waalimu wa Shule hizo, niombe sehemu iliyobakia Mkurugenzi wetu wa Manispaa aweze kuweka nguvu yake ili vyoo vianze ujenzi na wanafunzi wawe na sehemu rafki ya kupata huduma " Amesema Mhe. Tunda. 

Aidha, amewahakikishia Waalimu kuwa changamoto zinazowakabili zinatatuliwa kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo pamoja na Serikali ambayo ni Manispaa ya Morogoro wenye dhamana ya kusimamia huduma.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwere A akizungumza kwa niaba ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwere B, amemshukuru Mh.Tunda kwa kuchangia ujenzi wa Vyoo katika shule hizo.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media

SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL: chombo huru media.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.