Header Ads

MILIONI 120 KUJENMGA BWENI SHULE YA SEKONDARI MOROGORO


HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro inatarajia kuanza ujenzi wa Bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Morogoro lenye thamani ya Shilingi Milioni 120.

Kauli hiyo ameitoa , Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Gabriel Paulo, katika Kikao Cha Bodi ya shule  kilichofanyika Julai 06/2023 Cha kuchague eneo la ujenzi wa Bweni hilo.

Gabriel, amewataka wasimamizi wa mradi wa Bweni hilo kuwa waadilifu na Matumizi ya fedha za mradi huo.

Aidha, Gabriel, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha miundmbonu ya elimu na kukuza sekta hiyo kwa ujenzi wa Madarasa pamoja na kutoa fedha za Mabweni .

Kwa upande wa Kaimu Afisa Manunuzi Manispaa ya Morogoro, Ashura Juma , ameutaka Uongozi wa Shule kufuata sheria za Manunuzi ya vifaa vya ujenzi.

Aidha, ashura ameitaka Kamati ya mapokezi ya ujenzi kuwa makini na vifaa vinavyoshuka ili kukwepa udanganyifu.

Diwani wa Kata ya Boma, Mhe. Athumani Lujuo, amewataka watakao pata tenda ya ujenzi wahakikishe mradi huo unakuwa Bora na Viwango na kuendana na thamani ya fedha iliyotolewa.

Mwenyekiti wa Bodi,Ndg. Amiri Nondo, ameishukuru Manispaa ya Morogoro Kwa kuweza Kutatua kero ya Bweni katika Shule hiyo.

Nondo, amesema ujenzi huo wa Bweni unatarajia kuchukua jumla ya wanafunzi 80 na kupunguza 

Mkuu wa Shule ya Sekondari Morogoro, Mwl. Boniface Gonjo, amesema atahakikisha anasimamia Kamati za Ujenzi kwa ufanisi wa hali ya juu ili mradi huo ukamilike kwa wakati na kuwa na ubora Kama ulivyo kusudiwa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.