Header Ads

DIWANI BUTABILE AMPONGEZA DIWANI LATIFA KWA KUGAWA VITENDEA KAZI UWT KATA YA MAFIGA.

DIWANI wa Kata ya Mafiga Mhe. Thomas Butabile, amepongeza Mhe. Latifa Ganzel Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Morogoro kwa kugawa vitendea kazi Kwa Jumuiya ya Wanawake UWT Kata ya Mafiga.

Pongezi hizo amezitoa Julai 8/2023 katika ziara ya Diwani huyo wa Viti Maalum ya kufanya ziara kwa Matawi yote ya UWT Kata ya Mafiga akiwa mlezi wa Kata hiyo.

Mh. Butabile, amesema Mhe. Latifa, amekuwa mfano wa kuigwa kwani kitendo hicho cha kugawa vitendea kazi ni moja ya kuimarisha uhai wa Jumuiya hiyo.

Naye Diwani huyo wa Viti Maalum, Mhe. Latifa Ganzel, amesema lengo la kugawa vitendea kazi ni kuimarisha uhai wa Jumuiya na kuwakutanisha wanajumuiya hiyo kwa ajili ya kuwaweka pamoja.

" Hii ni ziara yangu nikiwa mlezi wa Kata hii, kwanza nimegawa vitendea kazi Kwa Uongozi wa Kata na Matawi, lakini nimegawa Cherehani kwa ajili ya kuitumia Kama kitega Uchumi kitakachowaingizia Mapato " Amesema Mhe. Ganzel.

Aidha, Mhe. Latifa, amesema vitendea kazi alivyovigawa kwa Viongozi wa Matwai wa UWT Kata ya Mafiga ni kwa ajili ya kurahisiha utendaji wao wa kazi huku akihidi kuendelea kuimarisha uhai wa Jumuiya hiyo.

Ziara ya Mhe. Ganzel, imekuwa ni muendelezo wa ziara zake katika Kata anazo zilea kwa lengo la kusikiliza kero na kuimarisha uhai wa Jumuiya.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.