KAMATI NDOGO YA AFYA MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KERO ZA VITUO VYA AFYA ZITATULIWE KWA WAKATI.
KAMATI ndogo ya afya Manispaa ya Morogoro ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Rashid Matesa, imefanya ziara ya kukagua miradi ya afya katika Manispaa hiyo na kuagiza Uongozi wa Manispaa kutatua haraka changamoto zinazojitokeza katika Vituo vya Afya.
Ziara hiyo imefanyika Julai 12/2023 huku msisitizo wa kamati hiyo ni kukamilika kwa wakati miradi ya afya ili ianze kutoa huduma.
Aidha, Kamati hiyo pia imetoa pongezi kwa Mkurugenzi na Wataalamu katika uendeshaji wa miradi kwa kuzingatia viwango ikiwemo ubora wa majengo pamoja na kasi ya uendeshaji.
Pia, hiyo imesisitiza kuwa katika changamoto zilizopatikana kwenye baadhi ya miradi kutiliwa mkazo kuhakikisha zinafanyiwa kazi ikiwa ni moja ya kazi ya kutimiza majukumu ya kamati.
Mwisho, Kamati hiyo, imemuagiza Mganga Mkuu wa Manispaa kuhakikisha katika Vituo vya afya na Zahanati zinapohitaji wauguzi basi wawapeleke kwa haraka ili huduma ziendelee kutolewa.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia, bila ya kuingia website
Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru_media
SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL: chombo huru media.
Post a Comment