BUTABILE AFICHUA SIRI YA UFAULU KIDATO CHA SITA MAFIGA 2023 .
DIWANI wa Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro, Mhe. Thomas Butabile, amesema matokeo ya ufaulu katika sekta ya elimu katika vipindi 3 vya Uongozi wake yanazidi kuimarika kutokana na mpango kazi waliojiwekea katika Ofisi yake ya Kata na Uongozi wa Shule.
Kauli hiyo ameitoa Julai 16/2023 ,kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha Sita mwaka 2023 ambapo shule ya Sekondari Mafiga imeendelea na rekodi yake ya ufaulu.
Akizungumza juu ya ufaulu wa Shule hiyo, Mhe. Butabile, amesema , jumla ya watahiniwa waliofanya mtihani kidato cha sita mwaka 2023 ni 163, na ufaulu daraja 1 wanafunzi 58, daraja 2 wanafunzi 95 na daraja 3 wanafunzi 10.
Aidha, amesema katika mwaka 2022, wanafunzi waliofanya mitihani ni 108, wanafunziu 60 walipata daraja la 1, wanafunzi 47 daraja la 2 na mwanafunzi 1 alipata daraja la 3.
Katika mwaka 2021 watahiniwa walikuwa 75, na waliopata daraja la 1 ni wanafunzi 40, daraja la 2 wanafunzi 35.
Mhe. Butabile, amesema matokeo hayo yanaifanya shule hiyo kuwa na uwiano mzuri wa ufaulu katika vipindi 3 mfululizo tangia aingie madarakani mwaka 2022.
" Matokeo upande wetu wa elimu Kat yetu ya Mafiga yanaridhisha sana ,sio upande wa Sekondari bali hata upande wa shule za Msingi, kwani upande wa shule ya Msingi katika wanafunzi wanafunzi 10 bora upande wa mitihani ya Moko Mkoa, miongoni mwao yupo mwanafunzi aliyetokea Shule ya Msingi Mafiga A Msichana, najivunia katika kipindi changu cha miaka 3 upande wa elimu yapo mengi nimefanya hususani upande wa ujenzi wa madarasa pamoja na maktaba ya kisasa Mafiga Sekondari , naamini tutaendelea kufaulisha kwani tutajipanga zaidi kuhakikisha kauli mbiu yetu ya Elimu 'ZERO NA UTORO HAIKUBALIKI ' inaishi kwa vitendo " Amesema Butabile.
Aidha, amemshukuru Rais wa Awamu ya Sita , Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya ustawi wa maendeleo ya elimu nchini.
Hata hivyo, Butabile, ameupongeza Uongozi wa Shule ya Sekondari Mafiga kwa kushirikiana na Afisa Elimu Kata kwa kuwa na mipango makini ya kuendeleza ufaulu shuleni hapo.
Amesema changamoto iliyopo katika Shule ya Sekondari Mafiga ni kujengewa uzio pamoja na ujenzi wa bwalo la chakula kwani wanafunzi ni wengi na eneo la chakula halikidhi huduma ya wanafunzi hao.
Mwisho, ametoa shukrani zake za dhati kwa Baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro, Mkurugenzi wa Manispaa na timu yake ya wataalamu kwa kazi kubwa ya kuiletea maendeleo Manispaa kwa kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo katika kufanikisha ndoto ya Manispaa kuwa Jiji.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia, bila ya kuingia website
Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru_media
SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL: chombo huru media.
Post a Comment