BARAZA la Mendeleo ya Kata (BMK) imeadhimia na kumtaka Afisa Elimu Kata kuhakikisha anasimamia taratibu zote ili Kamati za shule ziundwe.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa BMK, Diwani wa Kata ya Mafiga Mhe. Thomas Butabile, katika Kikao cha BMK kilichofanyika Julai 11/2023 Ukumbi wa Ofisi ya Kata hiyo.
Mhe. Butabile, amesema nafasi zote ambazo zipo wazi na shule ambazo hazina Kamati za Shule sasa ni wakati wa kwenda kuunda kamati hizo kwa kufuata utaratibu wa muundo wa kamati.
Aidha, Mhe. Butabile, amesema miongoni mwa umuhimu wa kamati za shule ni kusaidia kudumisha uhusiano mwema kati ya shule na jamii inayozunguka shule,husaidia ukusanyaji wa michango mbalimbali ya maendeleo ya shule kutoka kwa wanajamii, husaidia upatikanaji wa nyumba kwa shule ambazo hazina nyumba kwaajili ya kuishi walimu , husaidia kudhibiti na kudumusha nidhamu ya shule pamoja na kuwawakilisha wazazi , wanafunzi na walimu.
Hata hivyo ,ameziagiza Kamati za shule zitakazouundwa zihakikishe zinawashirikisha ipasavyo wazazi ili kuleta mabadiliko ndani ya kamati hizo pamoja na shule katika kufanikisha lengo la utoaji wa elimu bora shuleni.
"Katika kamati mtakazo ziunda natarajia kuona wajumbe wa kamati za shule wakiwashirikisha wazazi katika masuala mbalimbali yanayohitajika katika utatuzi na utekelezaji wa utoaji wa elimu bora shuleni" Amsema Butabile.
Katika hatua nyengine, BMK, imepitisha utaratibu wa kuwapima wanafunzi wakike Ujauzito kila baada ya miezi 3 ili kubaini mwanafunzi ana ujauzito au la .
"Hili litatusaidia sana, katika kipindi hiki ambacho tunapitia changamoto nyingi hususani unyanyasaji wa jinsia, ulawiti , niombe sasa twendeni tukawapime wanafunzi wetu wa kike ili tuweze kubaini kama wana ujazuito na kuchukua hatua za awali na huu ndio utakuwa utaratibu wetu ndani ya Kata kwa shule zote za Msingi rika ballehe na Sekondari " Amesema Mhe. Butabile.
Kuhusu suala la Bima ya afya, Mhe.Butabile, amewataka wasajili wa bima ya afya ya CHiF ilioboreshwa ngazi ya jamii kuongeza kasi ya uandikishaji kwa wananchi.
Aidha, amewataka watendaji wa Mitaa kwa kushirikiana na Wenyeviti wa Mitaa kuongeza nguvu ya kutoa elimu na kuwashirikisha wananchi katika kuchangia miradi ya maendeleo.
Kuhusu barabara za ndani, amesema kwa sasa mpango wake ni kuhakikisha barabara za ndani zinapitika kwa urahisi kwani tayari ameshafanya mazungumzo na watu wa TARURA kwa ajili ya ukarabati wa barabara korofi.
Post a Comment