Header Ads

JUMUIYA YA WAZAZI CCM KATA YA MKUNDI YAIOMBA SERIKALI KUTUPIA MACHO SHULE ZA PEMBEZONI.



JUMUIYA ya Wazazi CCM Kata ya Mkundi imeuomba Uongozi wa Manispaa ya Morogoro kutupia macho shule ya Msingi Sangasanga kutokana na uhaba wa madarasa.

Kauli za Viongozi hao wamezitoa Julai 20/2023 katika ziara ya Kamati ya Utekelezaji Wazazi CCM Kata ya Mkundi ya kukagua maendeleo ya Shule ya Msingi Sangasanga.

Akizungumza kwa niaba ya Kamati hiyo, Mwenyekiti wa Wazazi CCM Kata ya Mkundi, Ndg. Daud Msuya, amesema wakati Manispaa inatekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa itupie macho na shule hiyo ya Sangasanga pamoja na Ujirani shule ambazo zipo pembezoni.

Katika hatua nyengine, Jumuiya ya wazazi imewapongeza wananchi wa eneo la Sangasanga kwa kujitolea kuchimba shimo la choo la shule hiyo.

" Jumuiya yetu inahusika moja kwa moja na masuala mazima ya elimu, tumefanya ziara yetu ikiwa na lengo la kuona changamoto za elimu, bado shule zetu hizi za pembezoni za  Sangasanga na Ujirani zina uhaba wa Madarasa, tunaiomba Serikali hususani Mkurugenzi wa Manispaa kutupia jicho shule hizi za pembezoni, madarasa machache na madawati pia ni changamoto, lakini Viongozi wetu wa Mitaa tusimamie maendeleo ya shule hii bado muda upo wananchi ni wasikivu sana tukiwashirikisha wanashiriki katika ujenzi wa miradi ya maendeleo" Amesema Msuya.

Aidha, katika ziara hiyo, Jumuiya ya Wazazi iliweza kupokea taarifa ya shule ya Sangasanga na kuhaidi kuzifikisha changamoto zote katika vombo husika ili zifanyiwe kazi.

Katika hatua nyengine , Jumuiya hiyo, wamepata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi huku wakiendelea kuwatia moyo na kuwataka wasome kwa bidii.

Naye Katibu wa Wazazi CCM Kata ya Mkundi, Geofrey Mwatesa, amesema kama Jumuiya wataendelea na jukumu la kusimamia elimu pamoja na uhai wa Jumuiya.

Pia, wajumbe wa Kamati hiyo wamewapongeza waalimu wa shule hiyo kwani licha ya uwepo wa changamoto wanazokumbana nazo lakini wameendelea kufanya kazi kwa moyo mkubwa katika kunyanyua viwango vya ufaulu katika shule hiyo.

Mwisho, Mwenyekiti Msuya, ameiomba Serikali , Uongozi wa Kata ya Mkundi pamoja na wadau wa maendeleo kusaidia kupatikana kwa Pampu yenye uwezo wa kusukuma maji katika Kisima cha shule hiyo kwani Pampu iliyopo haina uwezo wa kusukuma maji vizuri.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.