VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA KATA YA UWANJA WA TAIFA WAHIMIZWA KUSIMAMIA USAFI WA MAZINGIRA
VIONGOZI wa Serikali za Mitaa Kata ya Uwanja wa Taifa Manispaa ya Morogoro, wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wananchi kufanya usafi wa mazingira kwenye maeneo yao pamoja na kufukia madimbwi yote ili kuteketeza mazalia ya mbu yanayopelekea kuongezeka kwa mbu na ugonjwa wa malaria.
Hayo yamesemwa Julai 19/2023 na Diwani wa Kata ya Uwanja wa Taifa ,Mhe. Rashid Matesa ,katika Kikao cha Baraza la Maendeleo la Kata (BMK) kilichofanyika Ofisi ya Kata hiyo.Matesa ,amesema kuwa Jamii inahitajika kuboresha usafi wa mazingira hivyo basi Viongozi wa Serikali za Mitaa wawajibike katika kuhimiza usafi wa mazingira.
“Kama mnavyojua Kata yetu tulikuwa na mdhabuni wa usafi Kajenjere, sasa mkataba wake umemaLizika , wakati Manispaa wakiendelea na mchakato wa kumpata mdhabuni mpya, niombe Wenyeviti wa Mitaa tuwe mstari wa mbele katika kusimamia usafi, baketi za kuwekea taka zipo,kikubwa wananchi walipe ada ya taka na kusimamia usafi ili mji wetu uwe safi na kuwapa ushirikiano wakusanyaji wa fedha za taka " Amesema Matesa.

Aidha, Matesa amesema usimamizi wa usafi ni muhimu kwani kufanya hivyo ni kutekeleza usimamizi wa Sheria ya Afya ya Jamii ya Mwaka 2009 na Sheria ya Usimamizi ya Mazingira ya mwaka 2004.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia, bila ya kuingia website
Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru_media
Post a Comment