Header Ads

DC NSEMWA AIPONGEZA MANISPAA YA MOROGORO KUVUKA MALENGO KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA CHANJO.



MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Rebeca Sanga, ameipongeza Manispaa ya Morogoro kwa kupitiliza malengo ya utoaji wa huduma za chanjo kwa wananchi.

Pongezi hizo amezitoa Julai 13/2023 katika Kikao  cha Tathmini ya utoaji huduma za chanjo kuanzia Januari -Desemba 2022 hadi Januari-Juni 2023 kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi Kuu ya Manispaa.

DC Nsemwa , amesema, chanjo huokoa maisha ya mama na mtoto kwa kumkinga dhidi ya maradhi ambayo yanazuilika, na kuongeza kuwa kupata chanjo ni jambo la lazima kwavile inalinda pia kizazi kijacho dhidi ya magonjwa mbalimbali kama Surua na Polio.

Ni wajibu na jukumu la kila Mzazi kuhakikisha mtoto wake anapata chanjo kwani ni muhimu kwa afya na inazuia watoto kupata ugonjwa wa kupooza,wakina watendaji nendeni mkasimamie hili na kuwakumbusha amewaomba wakina Baba kujenga tabia ya kuwasindikiza wake zao Vituo vya afya pamoja na kuwasisistizia  wakina mama kuhakikisha wanapata chanjo zote kipindi cha ujauzito na wanapojifungua na kuhakikisha mtoto aliyezaliwa anapatiwa chanjo zote za utotoni ili kumlinda na maradhi kwani chanjo hizi ni salama na hazina madhara yoyote Kiafya”.Amesema DC Nsemwa.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro , Dr. Charles ,Mkumbachepa, amesema mikakati ambayo imefanikisha kuvuka lengo la utoaji chanjo ni kuwafikia  walengwa katika matamasha na maadhimisho mbalimbali .

Naye Mratibu wa Chanjo Manispaa ya Morogoro , Philipo Bwisso, amesema Manispaa ya Morogoro imefanya kampeni ndogondogo 5 za chanjo ya UVIKO-19 na kufanikiwa kutoa chanjo kwa walengwa 249367 sawa na asilimia 106 kufikia Machi ,2023.    

Bwisso,amesema kuwa Manispaa ya Morogoro vituo 87vinatoa huduma za afya , vituo 55 (63%) vinatoa huduma za chanjo. Kuhusu Chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi, amesema asilimia imepanda kutoka asilimia 80 januari -Desemba 2022 hadi kufikia asilimia 124 Januari-Juni 2023.

"""Ratiba ya chanjo ni kila siku za kazi kwa vituo vyote vinavyotoa huduma za chanjo,chanjo tunazo toa ni chanjo dhidi ya kifua kikuu kwa watoto (BCG), Dondako, pepopunda na kifaduro  (DTP), Polio ya matone (BOPV), Polio ya sindano (IPV), Pepopunda na Dondakoo kwa wajawazito (TD), Saratani ya mlango wa kizazi (HPV),Chanjo dhidi ya vichomi kwa watoto (PCV-13), chanjo dhidi ya kuhara (ROTAVAC), Surua Rubela (MR) pamoja na Chanjo ya UVIKO-19.

A  Aidha Bwisso, amezitaja changamoto wanazokumbana nazo wakati utoaji wa huduma ya chanjo zikiwemo uhaba wa majokofu na masanduku ya kusafirishia chanjo, mabadiliko ya hali ya hewa, hali ya kijiografia kwa baadhi ya maeneo pamoja na usafiri kwa ajili ya shughuli za usimamizi shirikishi na usambazaji wa chanjo kwenda vituoni.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.