EGG TANZANIA YAZIKUTANISHA ASASI ZA KIRAIA KUJADILI MICHANGO YAO KATIKA MAENDELEO YA JAMII.
ASASI za Kirai Manispaa ya Morogoro zimeketi pamoja katika kikao cha ujadili Michango yao katika maendeleo ya Manispaa ya Morogoro katika kuwatumikia wanajamii.
Kikao hicho kilichoandaliwa na Taasisi ya EGG Tanzania chini ya Mkurugenzi wake , Jumanne Mpinga, kimefanyika katika eneo la Ofisi ya EGG Tanzania Julai 28/2023.
Akizungumza katika kikao hicho, mgeni rasmi wa kikao ambaye ni Mstahiki meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amesema mchango unaotolewa na asasi za kirai katika Manispaa ya Morogoro ni mkubwa hivyo Asasi zinapaswa kubaki katika njia inayostahili.
Mhe. Kihanga ,amesema kuwa endapo asasi za kiraia zitakuwa haziwajibiki vyema watakaoathirika ni wananchi ambapo itawapa wakati mgumu kupata uchambuzi wa kina kuhusu masuala mbalimbali.
Naye Mkurugenzi wa EGG Tanzania, Jumanne Mpinga, amesema kuwa lengo la kuwakutanisha Asasi na Madiwani ni kujadili mambo mbalimbali ya kijamii na kujengeana uwezo na uwelewa wa pamoja wa namna gani Asasi hizo zitakavyoweza kusaidia jamii na kushirikiana na Serikali .
Mpinga , amesema EGG Tanzania ni Taasisi ambayo imekuwa ikishiriki moja kwa moja katika kutatua matatizo ya kijamii katika Sekta ya Elimu , Afya pamoja na huduma ya Maji ( uchimbaji wa Visima).
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Asasi za Kiraia Mkoa wa Morogoro (UNGO) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Agriwezesha , Deograsia Chuma, amesema kuwa asasi za kiraia zimekuwa na mchango mkubwa katika utawala wa sheria ikiwa katika mabadailiko ya sheria mbalimbali nchini kwani wamekuwa wakishirkishwa katika mijadala ya Kitaifa.
Miongoni mwa Madiwani wa Manispaa ya Morogoro , Diwani wa Kata ya Mindu, Mhe. Zuberi Mkalaboko, ameziomba Asasi hizo zishuke kwa Viongozi wa Kisiasa ambao ndio wana wananchi badala ya kufanya kazi na watendaji pekee jambo ambalo litaendelea kuwapa ugumu katika majukumu yao na kushindwa kujua vipaumbele vya wananchi katika sehemu husika.
Katika hatua nyengine, Mkurugenzi Mtendaji wa UECO, Sophia Kalinga, ameishauri Taasisi ya EGG Tanzania, kusaidia Asasi ndogo zinazojishughulisha na masuala ya elimu ili zifikie mafanikio kama ilivyo kwa EGG Tanzania.
Post a Comment