Header Ads

BUTABILE AWAHAKIKISHIA WANANCHI WA MTAA POLISI NA MSUFINI UKARABATI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA.


DIWANI wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile, amewahakikishia Wananchi wa Mtaa wa Polisi na Msufini kuikarabati barabara inayopita katika Mitaa hiyo.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 09/2023 katika Mkutano wa Wananchi wa Mitaa hiyo miwili.

Butabile, amesema barabara hiyo ni korofi hivyo amejipanga kushirikiana na Uongozi wake wa Kata kuhakikisha miundombinu ya barabara hiyo ina karabatiwa.

" Tupo hapa katika kikao kwa agenda kuu ya barabara, ukiangalia hii barabara ni korofi, hivyo Mpango wangu ni kuifanyanyia maboresho ili iweze kupitika vizuri hususani kipindi Cha mvua" Amesema Mhe. Butabile.

Aidha, amesema kikao kijacho Cha tarehe 15/7/2023 atawaleta Wataalamu kutoka TARURA kwa ajili ya hatua za upembuzi yakinifu ili ukarabati huo uanze mara moja.

Hata hivyo, Mhe. Butabile, amewataka Viongozi kutimiza wajibu wao hususani katika kuwashirikisha Wananchi katika kuchangia miradi ya Maendeleo.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.