Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro awakumbusha Wauguzi kuzingatia maadili ya kazi.
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro , Sheilla
Lukuba, amewakumbusha Wauguzi Manispaa ya Morogoro kutoa
huduma kwa kuzingatia kanuni na taratibu kama walivyojifunza.
Hayo ameyasema leo Mei 12, 2020 Ofisini kwake, mara baada ya
mahojiano na waandishi wa habari juu ya kuadhimisha Siku ya Uuguzi Duniani
ambayo hufanyika Mei 12, kila mwaka.
Aidha, amewataka ,Wauguzi kuendelea kutekeleza majukumu ya kazi kwa kuzingatia
kanuni na taratibu za kitaaluma kwa lengo la kutoa huduma bora za afya kwa
wagonjwa.
Hata hivyo, amewakumbusha wauguzi kuzingatia mafunzo yanayotolewa mahala pa kazi kwani ndio
yanayochochea kutoa huduma bora ya afya kwa wagonjwa.
Amewataka wauguzi kutambua kwamba huduma wanayotoa kwa wagonjwa
ni huduma ya kibinadamu kwani elimu inachangia kufikia malengo ya kutoa huduma
bora.
“Hivi sasa mambo yetu yanakwenda vizuri. Juzi juzi wakati wa Uzinduzi wa Wodi ya wazazi Regina Chonjo Sabasaba , tulipata
ripoti nzuri ya kuhusu wakina mama wanao jifungua katika Vituo vyetu vya afya
kupitia taarifa ya Kituo cha afya cha Sabasaba, ni jambo jema na mmeonyesha ni
jinsi gani mlivyo makini katika utendaji wenu wa kazi, Malalamiko mengi
yamepungua lakini ukifuatilia utabaini
kwamba malalamiko mengi ni ya wagonjwa au mgonjwa kutaka kupewa kipaumbele
kupata huduma ya afya badala ya kufuata utaratibu, tuwe makini na tufanye kazi
hii kwa moyo mmoja na kama kuna changamoto ipo sehemu ya kusemea na kusikilizwa tunataka Manispaa yetu iwe mfano katika
utoaji bora wa huduma na wananchi wafurahie na kuja kwetu badla aya kuhamia
katika Hospitali binafsi ” amesema Lukuba..
Lukuba, amewapongeza wauguzi kwa kutekeleza majukumu ya kutoa
huduma za afya kwa kuzingatia taratibu za kitaaluma kwa asilimia 100.
Katika hatua
nyengine, amepinga vikali vitendo vya udhalilishaji kwa wauguzi huku akitaka vifanyiwe
kazi kwa kuwa vitendo hivyo vinawapunguzia ari ya kufanya kazi.
“Sijawahi kupata
malalamiko haya lakini kama vitendo hivi vipo katika Manispaa yetu iwe mwiko na
ni marufuku , vikitokea na tukambaini aliyefanya vitendo hivi tutamchukulia
hatua kali za kisheria, kwani lengo ni kuwahudumia wananchi wetu kwa ari kubwa
sasa tukiwa na vitendo hivi vya udhalilishaji tunawapunguzia ari ya kufanya
kazi Waauguzi wetu” Ameongeza Lukuba.
Amesema bado ipo haja
ya kuendelea kuwapatia wauguzi mafunzo
mbalimbali ambayo yatawasaidia zaidi kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa.
Naye, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr. Ikaji Rashidi, amewataka wauguzi kutoa taarifa kwa uongozi wa
Manispaa endapo watadhalilishwa wakati
wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili watakaobainika wachukuliwe hatua za
kisheria.
“Mmesikia jamani nendeni mkawaeleze wenzenu kwamba endapo
muuguzi atadhalilishwa, bila kuchelewa naomba atoe taarifa kwa uongozi ili
wanaofanya hivyo tuwafikishe mbele ya vyombo vya dola,” amesema Dr.
Ikaji..
Maadhimisho hayo
hufanyika Mei 12, kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Wauguzi Sauti
inayoongoza Afya kwa Wote.” Mwaka huu kitaifa maadhimisho yanafanyika mkoani
Katavi.
Post a Comment