DC Chonjo aikabidhi Manispaa Morogoro Ambulance yenye thamani ya Shilingi milioni 45 iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe.Abood .
Mchungaji wa Kanisa la Faith Baptist Church lilopo Kola "B" , Mchungaji Jerry Max Wyatt (kulia) akikabidhi msaada wa Vitakasa mikono, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, amepokea
Ambulance yenye thamani ya Shilingi milioni 45 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la
Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood kwa ajili ya Wananchi wa Manispaa ya Morogoro.
Tukio hilo la kukabidhi
gari la Wagonjwa (Ambulance) limefanyika leo Mei 18,2020 kwenye Kituo
cha afya Sabasaba Manispaa ya Morogoro .
Akizungumza na Waandishi wa habari,amemshukuru Mbunge wa
Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood , kwa kutekeleza ahadi ya kukabidhi
gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa ajili ya wananchi wake wa Jimbo
la Morogoro Mjini ili waendelee kupata
huduma bora pale wanapohitajika kupatiwa matibabu wanapokuwa na maradhi.
“ Nina mshukuru sana Mhe. Abood ,kwa kuwa pamoja na wananchi
wake, niseme tu wabunge wengi wangekuwa wanatekeleza ahadi zao kwa wananchi na
kuwa karibu na matatizo ya wananchi kama ilivyo kwa Mhe. Abood ,naamini tungefikia wakati
wakuweka kikomo cha ubunge na tungesema hakuna tena kampeni za uchaguzi “
Amesema DC Chonjo.
DC Chonjo ,amesema kuwa Mhe. Abood amekuwa akijitolea kwa
mambo mengi hususani katika kuwatatulia changamoto wananchi wa Jimbo lake.
“ Tumeona hata katika risala iliyosomwa na Mganga Mkuu wa
Manispaa ya Morogoro ya ujenzi wa Duka la
Dawa la Kituo cha afya sabasaba , amesema pesa ya kuunganisha umeme laki 5
atamalizia yeye licha ya kuwa anamuuguza mama yake Afrika Kusini , nimeongea
nae asubuhi amesema kama kuna matatizo madogo madogo tumwambie atayafanyia kazi
hapa inatudhihirisha ni kwa namna gani Mbunge wetu alivyo karibu na wananchi
wake , ni wabunge wangapi wanaweza kujitolea pesa zao za mfukoni kwa ajili ya
wananchi,naendelea kumpongeza sana Mwenyezi Mungu amlinde huko aliko na warudi
salama hapa nchini” Ameongeza DC Chonjo.
Aidha amesema Mhe. Abood ,amekuwa akipambana sana katika
mapambano ya Ugonjwa wa Corona hata ukiangalia katika maeneo mbali mbali
ikiwemo masoko, mtaani na vijiwe vya bodaboda kote amegawa ndoo za maji,sabuni, barakoa na Vitakasa mikono kwa
kutumia pesa zake binafsi na sio za mfuko wa Jimbo ambapo hii yote ni kuonyesha anajali afya za
wananchi wake.
Hata hivyo, amewaomba Wananchi wa Jimbo la Morogoro waendelee kumuombea kwani
sio rahisi mtu ana muuguza mzazi wake na yupo kwenye matatizo lakini anakumbuka
ana jukumu jengine la kuendelea kuwahudumua wananchi wake japo mwenyewe hayupo.
Pia, amemuomba Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro,
kumkabidhi gari hilo la wagonjwa kijana ambaye ni makini na atakayechukulia
gari hilo kama mali yake lenye kumpatia kipato na familia yake , ambapo anatakiwa atambue kwamba anajukumu la kuitunza kwa kuwa gari hilo ni la gharama na linatumika katika kuokoa maisha
ya watu.
Amesema kuna madereva
wengine kwa sababu wanajua wanaweza
kupita mahala popote kwa king’ora unakuta wajanja wakimrubuni kesho utasikia
limekutwa Ulanga limebeba bangi kwani matukio haya ni kawaida na yanatokea ,
hivyo ameomba gari hilo lichungwe na kufanya kazi amabayo imekusudiwa kufanya
kwa wananchi wa Manispaa ya Morogoro.
Katika hatua nyengine, amewapongeza wadau mbali mbali
ikiwemo taaisis ya Kinara For Youth
Evulution pamoja na Kanisa la Faith Baptist Church lililopo Kola ‘B’ Kata ya
Bigwa kwa kujitolea vifaa tiba vya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA .
Hata hivyo,Kaimu Meya Manispaa
Morogoro na Diwani Kata ya Boma, Mhe.Amiri Juma Nondo, amesema kitendo alichofanya Mhe. Abood
kimeonyesha kwamba ni jinsi gani anaguswa na matatizo ya wananchi.
“ Mbunge wetu amekuwa karibu sana na wananchi wake, mtu
ambaye anatumia fedha zake za mfukoni badala ya kutumia na familia yake ana
jinyima kwa ajili ya wananchi huyo ni kiongozi bora na sisi wana morogoro
tunamuomba Mwenyezi Mungu aweze kumponya na maradhi pamoja na mzazi wake warudi salama
waendelee na majukumu ya kuwatumikia wananchi na Taifa kwa ujumla” Amesema Mhe.
Nondo.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Sheilla Lukuba,
amempongeza Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood kwa msaada
wa gari la wagonjwa huku akiahidi kulitunza na kuwahudumia wananchi kama ilivyokusudiwa.
Lukuba amesema gari hilo japo limetolewa katika Kituo cha
afya cha sabasaba lakini litatumika katika kuwahudumia wananchi wote wa
Manispaa ya Morogoro.
“ Tunampongeza sana Mbunge wetu, kwakweli ni wabunge
wachache wenye uthubutu wa kutumia fedha zao za mfukoni ambazo wangeweza kula
na familia , lakini ameona ni vyema akatoa sehemu ya pato lake kwa ajili ya wananchi wake ili waweze kupata huduma
bora pale wanapopatwa na maradhi, niwaombe watumishi na dereva atakayekabidhiwa
gari hili mulitunze , sio baada ya mwezi
mmoja gari halitamaniki , tulitunze ili liendane sawa na lengo tarajiwa “
Amesema Lukuba.
Amesema kuwa, kupatikana kwa gari la wagonjwa (Ambulance )
ambayo Mhe. Abood ameikabidhi kutatatua changamoto ya rufaa kwa wakina mama
wajawazito na wagonjwa wengine.
Kwa upande wa Katibu
wa Mbunge ambaye ametumia nafasi ya kumwakilisha, Ndg. Mourice Masala,
amesema Mhe. Abood amelitoa gari hilo kwa ajili ya Wananchi wa Manispaa ya
Morogoro.
Amesema pamoja na kutambua chanagamoto katika sekta ya afya,
ameona ni vyema akatumia fedha zake kununua
gari hilo lenye thamani ya shilingi milioni 45 liendeleee kutoa huduma kwa
wananchi na kuokoa maisha ya watu pindi wnapofikwa na maradhi.
“Mbunge wetu ,Mhe. Abood, amenituma nitoe salama zake na
amesema gari hilo litumike kwa malengo yaliyokusudiwa, anatambua changamoto
katika sekta ya afya, hata wakati wa risala ya mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro ya ujenzi wa duka la dawa, niliwasilianan nae
akasema kama kuna chanagmoto ndogondogo tumwambie na amesikia kwamba kuna dua
la dawa linajengwa hivyo ameahidi kutoa kiasi cha shilingi laki 5 kwa ajili ya
gharama za kuingiza umeme” Amesema Mourice.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr Rashidi Ikaji,
amesema Kituo cha afya cha sabasaba kinawahudumia wananchi 12,821 ambapo kiuhalisia
kituo hicho kinawahudumia wakazi wa ndani na nje ya Manispaa ikiwemo Wilaya za
Jirani kama Morogoro Vijijini na Mvomero.
Amesema kabla ya kuwepo kwa gari hilo, kituo kilikuwa
kikipata changamoto kubwa ya usafiri wa kuwawahisha wateja wa rufaa kwa wakati
katika Hospitali ya Mkoa hali ambayo ilikuwa inapelekea wakati mwengine wakina
mama kukosa watoto.
‘”Tuna mshukuru sana
Mbunge wetu Mhe. Abood kwa msaada huu, matuamaini yetu kwamba gari hili
litasaidia kupunguza vifo vya wakina mama na watoto wachanga kama si kumaliza
kabisa tatizo hili, tunampongeza sana kwa jitihada zake za kuwajali wanawake na
wapiga kura wake kwa ujumla” Amesema Dr. Ikaji.
Post a Comment