Katibu CCM Wilaya Morogoro Mjini awataka Madiwani kuwaeleza Wananchi Serikali ilichowafanyia katika Kata zao.
KATIBU wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Morogoro Mjini, Sofia Kibaba, amewataka Madiwani kuamka
usingizini na kuwaeleza Wananchi mambo ambayo Serikali imewafanyia katika Kata zao.
Kauli hiyo ameitoa Mei 19,
2020, katika Semina ya Mafunzo ya Maadili kwa Madiwani wa Manispaa ya Morogoro
iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kigurunyembe.
Akizungumza na Waandishi
wa habari, Kibaba, amesema Wanasiasa mtaji wao ni wananchi hivyo wana kila
sababu Madiwani kuwaeleza Wapiga kura wao ni mambo gani yametekelezeka katika
kipindi cha miaka 5, tangia wapate
nafasi ya kuchaguliwa katika uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2015.
Amesema kama Madiwani
wataendelea kukaa kimya , Chama Cha Mapinduzi au Madiwani itakuwa ni vigumu kwa
Wananchi kushindwa kujua ni mambo gani Serikali imewafanyia katika miaka yote
mitano tangia 2015/2020.
“Madiwnai waamke sasa,wote
tunafahamu kuwepo kwa ugonjwa wa CORONA , lakini sio lazima wakae katika
msongamano, hata wakiongea na Wajumbe wa Serikali za Mitaa, Wenyeviti wa Mitaa
yao kwa awamu , wakikutana na wazee maarufu na ile mikutano iliyoruhusiwa
haitakuwa jambo baya, kikubwa njia hizo itakuwa ni salamu tosha kwa wananchi
kujua nini Serikali yao imewafanyia katika maeneo yao na itawasafishia
njia Chama na wale wenye mpango wa
kurudi tena katika nyadhifa,” Amesema Kibaba.
“ Tunafahamu kuna utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa upande wa Kitaifa, Kimkoa, Kiwilaya na hata
katika upande wa ngazi ya Kata ambapo yapo mambo ambayo ameyatekeleza katika
kipindi chote cha miaka mitano, kwa sababu muda sio mrefu wanakwenda kumaliza
muda wao na Baraza la Madiwani litavunjwa na wataonekana kama wananchi wa
kawaidia na hatoweza kuonana na wananchi tena hadi taratibu za Chama
zitakotangazwa, ni jukumu lao sasa kuwaeleza wananchi mambo ambayo waliyaahidi
kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 , vingapi wamevitekeleza ili wananchi wawe na
uelewa wa nini Serikali ya Chama Cha Mapinduzi Chini ya Mhe. Dkt John Magufuli
vimefanyika katika kipindi hiki “ Ameongeza Kibaba.
Katika hatua nyengine,
Kibaba, amewataka Madiwani wahakikishe wananzingatia suala la maadili huku
akisema Diwani yeyote amabye atakwenda kinyume na maadili ndani ya Chama na
kama Diwani atachukuliwa hatua kali za kisheria kwa mujibu wa utaratibu ndani
ya Chama.
Post a Comment