Meya Manispaa ya Morogoro awataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Uboreshaji wa Daftari la wapiga kura.
Mhe. Kihanga akikagua majina yake kwenye Kituo cha Modeco 'B'.
Mhe. Kihanga akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuhakiki taarifa zake katika Daftari la Uboreshaji la wapiga kura . |
Mhe. Kihanga, akinawa maji na sabuni baada ya kuwasili katika Kituo cha kujiandikishia . |
Muhudumu wa Uchaguzi akimnyunyizia Mwananchi Kitakasa mikono baada ya kuwasili katika kituo cha kuhakiki taarifa . |
Wananchi wakiendela kuhakiki majina yao katika Moja ya Kituo cha Kujiandikishia cha Modeco 'B' Kata ya Mazimbu.
MSTAHIKI
Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga,
amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Awamu ya pili ya Zoezi la Uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuwahimiza Wananchi waliotimiza miaka 18 na wale ambao
walishajiandikisha awamu ya kwanza wajitokeze
kwa wingi kuhakiki taarifa zao ili kutimiza haki zao za kuwachagua viongozi
wanaowataka katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka 2020.
Kihanga
, ameyasema hayo leo Mei 2, 2020 Kwenye Ofisi ya Kata ya Mazimbu wakati alipokwenda kuhakiki taarifa zake kwenye
Kituo alichojiandikishia kilichopo Mtaa wa Modeco 'B' .
Aidha, amewata
Madiwani wote kutumia fursa hii kuwaagiza Wenye Viti wao wapitie nyumba hadi
nyumba kuwahimiza Wananchi wao kwenda kuhakiki taarifa zao kwani muda uliopo sio rafiki.
“Tuna
muda mchache sana, leo Jumamosi na Jumapili ni siku za mapumziko , kwa Wafanya
kazi na wale watumishi wazitumie siku hizi kikamilifu kuhakiki taarifa zao ili
itakapoanza Jumatatu siku za kazi basi waendelee na majukumu yao mingine , muda
sio rafiki kwentu siku hizi 3 sio nyingi sana, niwaombe tusidharau lazima
mtambue kwamba zoezi hili ni muhimu sana , mimi nimehakiki taarifa zangu lakini
Picha haipo kwahiyo ikanibidi nikapige picha upya na kupewa kitambulisho changu
kipya, ukidharau unaweza ukajikuta unapoteza sifa za mpiga kura katika uchaguzi”
Amesema Kihanga.
“Zoezi hili limeanza lazima Wananchi walipe kipaumbele na
kuacha dharau, napenda kuwaomba Wananchi wa Manispaa ya Morogoro kwenye Kata
zote 29, wajitokeze kwa wingi kwani zoezi hili linahusika na uandikishaji wa
wapiga kura wapya wenye sifa ili waweze kupata fursa za kushiriki kupiga kura
katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka 2020”
Amesisitiza Kihanga.
Pia amewaomba wale wananchi waliohama kutoka eneo moja
kwenda jengine waende katika Vituo walivyopo kwa sasa ili waweze kuhamisha
taarifa zao katika Daftari la wapiga kura ili waweze kushiriki kikamilifu
katika kuwachagua Viongozi katika uchaguzi Mkuu.
Hata hivyo, amesema wapo wale ambao wamefikisha umri wa miaka 18
au wanafikisha mwaka huu kabla ya Mwezi Oktoba, waende katika Vituo ili waweze
kurekebisha taarifa zao na wale ambao
wamehama Mkoa, eneo nje ya Kata pamoja na kutoka Jimbo moja kwenda jengine wote
wanatakiwa wakahakikihi taarifa na kuweza kuhamisha taarifa zao.
Hata hivyo ameendelea kutoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya Morogoro kuendelea kufuata ushauri wa Wataalamu wa Afya katika kujikinga na Ugonjwa wa Corona ikiwemo kunawa Maji tiririka na sabuni, kutumia Vitakasa mikono ( Sanitizer), pamoja na kuepuka msongamano isiyo ya lazima na kukaa nyumbani kama mtu hana sababu ya Msingi ya kutoka
Naye , Afisa
Mwandikishaji Msaidizi wa Jimbo Morogoro Mjini, Waziri Kombo , amesema bado
hajaridhishwa na Mwitiko wa watu , hivyo amewataka Wananchi kuacha kupuuzia
swala hilo kwani wasipofanya hivyo kuna hatihati ya wale ambao taarifa zao
hazitakuwa sahihi au kutoonekana kwa picha zao wakapoteza sifa ya kupiga kura.
Katika hatua nyenge,
Kombo,amesema kumekuwa na changamoto ya kutoonekana kwa picha za watu katika
Vituo, hivyo wananchi wanatakiwa watambue uhakiki ni jambo muhimu sana ili
waweze kuwa na sifa za kupiga kura.
“Serikali inajicho pana ,
ndio maana kuna zoezi la uhakiki, ukiangalia changamoto kubwa ambayo nimeiona
ni kutokuonekana kwa picha za watu katika majina yao waliyojiandikisha mwanzo, niwaombe wale ambao wanashida hiyo wakapige picha upya kwenye vituo vilivyowekwa, na uhakiki pia ni muhimu ili changamoto hii iweze kupatiwa ufumbuzi ,
kama tutadharau ujue kabisa utajipotezea sifa ya kuwa mpiga kura na kukosa haki
yako ya msingi na ya kikatiba” Amesema Kombo.
Kombo, amewataka
waandikishaji kushiriki
kikamilifu katika zoezi hilo la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura awamu
ya pili na kutekeleza zoezi hilo kwa kwa umakini na ufanisi pamoja
na utunzaji wa vifaa vyote vitakavyohusika katika zoezi hilo.
Amesema
matarajio yake ni kuona zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
wapiga Kura linafanikiwa kwa kiwango kikubwa ili kuwa na taarifa sahihi za
wapiga Kura.
Pia amesema njia mbadala zitakazotumika katika uhakiki wa daftari ni kama zifuatazo;
I. Bonyeza *152*00#ok
II. Chagua Namba 9 ambayo ni Uchaguzi Mkuu
III. Chagua tena Namba 1 ambayo ni Uhakiki Taarifa za Mpiga Kura
IV. Baada ya hapo unatakiwa kuingiza Namba ya Mpiga Kura (Utaweka Namba peke yake bila ya herufi (T) wala , Dash (-)
Kwa
upande wa Afisa Mtendaji wa Kata ya Mazimbu, Bi. Prisca Mawala, amesema kwa
upande wa Kata ya Mazimbu wamewahamasiha sana Wananchi kwa kutumia gari la
mapatangazo hivyo matarajio yake hizi siku mbili mahudhurio yataongezeka huku akiomba uhamasishaji zaidi kupitia kwa Wenyeviti wa Mitaa na wajumbe
wao.
Post a Comment