Manispaa Morogoro yaja na suluhisho la kupunguza usumbufu kwa wananchi kufuata dawa maduka binafsi.
Ujenzi wa Duka la Dawa Kituo cha Afya Sabasaba ukiendelea. |
HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro, imeaamua kutekeleza kwa
vitendo agizo la TAMISEMI la kutaka kila Halmashauri kuwa na Duka la dawa.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Mganga Mkuu wa Manispaa
ya Morogoro ,Dr Ikaji Rashid, amesema mara baada ya kukamilika kwa mradi huo ,utasaidia kurahisisha upatikanaji wa dawa kwa wakazi wote wa Kata 29 za
Manispaa ya Morogoro .
Dr. Ikaji, amesema , faida nyengine ya mradi utasaidia
kupunguza usumbufu wa wateja kufuata dawa maduka binafsi na kuongeza mapato ya
kituo na Halmashauri kwa ujumla.
Aidha, amesema kuwa kwa mujibu wa tathmini ya BoQ , mradi huo
utakapokamilika unategemea kugharimu kiasi cha Tshs Milioni 24,572,054/=
“Tumetekeleza agizo la TAMISEMI la kutaka kila Halmashauri
kuwa na Duka la dawa kwa kutumia mapato ya ndani ya Kituo hiki cha afya ,
lakini pia duka hili la dawa litakuwa mkombozi kwa wananchi wetu wa Manispaa
kwa ajili ya kupata dawa kwa bei halisi ya Serikali na kuwapunguzia umbali
mrefu na usumbufu wateja wetu kufuata dawa kwenye maduka binafsi, mpaka sasa
mradi huu umetekelezwa kwa asilimia 85% na ujenzi upo kwenye hatua ya mwisho ya
umaliziaji ambapo kazi zilizo bakia ni upigaji wa rangi, kuunganisha umeme,
mfumo wa Elektroniki na samani” Amesema Dr. Ikaji.
Hata hivyo, amesema kutokana na Ugonjwa wa CORONA mapato ya
kituo kwa sasa yameshuka pamoja na kituo hicho kuelemewa na gharama kubwa za
ukarabati na ununuzi wa vifaa vya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA kwa watumishi
.
“”Tumebakiza sehemu ndogo ya ujenzi, tunaomba msaada wa Mbunge
wetu wa Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood na Mkurugenzi wa Manispaa na wadau
mbalimbali watusaidie ili kukamilisha mradi huu kwa kazi ambazo zitagharimu
jumla ya shilingi Milioni 16,265,100/=” Ameongeza Dr. Ikaji.
Amesema miongoni mwa vitu vinavyohitajika
katika kukamilisha ujenzi uliobakia ni pamoja na kuweka mfumo wa Elektroniki
wenye thamani ya shilingi, 4,499,000/=, Samani (Shelf na kabati za Aluminiamu
Tshs 9,021,100/=, Kiyoyozi (AC) Tshs 1,800,000/= pamoja na Gharama za
kuunganisha umeme katika duka Tshs 445,000/=.
Katika hatua nyengine, amesema amesema Kituo kimefanya
ukarabati mkubwa wa vyoo na mfumo wa maji taka ndani ya Kituo na kuunganisha
mfumo huo kwenye mtandao wa maji taka wa MORUWASA ambapo mpaka sasa tayari
Kituo kimeunganishwa kwenye mtandao.
Amesema Kituo kimeanza ukarabati wa Kitengo cha kinywa na
meno ambapo katika Mnaispaa huduma hii hutolewa katika Kituo hicho na ukarabati
huo unalenga kuboresha huduma hizo na kukifanya kitengo hicho kuwa cha mfano
katika Manispaa ya Morogoro .
Amesema Vifaa vya kisasa kwa ajili ya kitengo hicho
vimeshaagizwa kupitia MSD huku ukarabati wa kitengo hicho pamoja na ununuzi wa
vifaa utagharimu Tshs milioni 72,000,000/= ambapo chanzo cha fedha hizo za
ukarabati zimetoka katika mfuko wa pamoja (Basket Fund).
Mwisho, amesetoa shukrani za kipekee kwa niaba ya Watumishi wa Kituo cha Afya Sabasaba,
Mhe. Diwani wa Kata ya Sabasaba na kamati ya usimamizi kwa Mbunge wa Jimbo la
Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood kwa kuwapatia gari pamoja nafedha za
kuunganisha Umeme kwenye duka la dawa ambapo amesema matukio hayo yatabakia
kuwa kumbukumbu kubwa isiyofutika kwa
Kituo cha afya pamoja na Manispaa kwa ujumla.
Post a Comment