Mkurugenzi Manispaa Morogoro awakumbuka Watoto Yatima kwa kugawa vyakula Makao ya Dar Ul Muslimeen kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias, akigawa Tende. |
MKURUGENZI
wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amegawa vyakula katika
Makao ya kulelea Yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili kuweza
kuwasaidia katika mfungo wa Mwezi Mtukufu Wa Ramdhani.
Tukio hilo la ugawaji vyakula limefanyika leo, Mei 8, 2020 katika Makao ya Dar Ul Muslimeen .
Tukio hilo la ugawaji vyakula limefanyika leo, Mei 8, 2020 katika Makao ya Dar Ul Muslimeen .
Akizungumza
baada ya kugawa vyakula hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro,
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa Morogoro, Bi. Sidina Mathias amesema vyakula
hivyo amevitoa kutokana na kuguswa kwake na watoto wanaoishi katika mazingira
magumu hususani katika kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Sidina,
amesema miongoni Mwa vyakula
vilivyotolewa na Mkurugenzi ni pamoja na Tambi Kg 25 ,nazi, Viazi vitamu, mihogo,
malimau, pilipili manga, sabuni ya unga , maharage Kg 20, mafuta ya kupikia,
sabuni, unga wa sembe Kg 25, sabuni ya mnala, Unga wa ngano Kg 25, tende huku akiahaidi kuleta sukari ya kilo 25 baada ya kupatikana.
"
Huu ni Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani, Mkurugenzi wetu wa Manispaa kwa kuguswa na
watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu yeye binafsi ameona
ni vyema katika kipindi hiki cha mfungo akawapatia kile alichonacho ili
kuendelea kuwaunga mkono wale amabao wamekuwa wakiwalea siku zote , ametoa
vyakula hivi sio kwa Vituo vyote bali ni vituo ambavyo vimekuwa vikimilikiwa
chini ya Taasisi za kislamu ili watoto
hao i wafunge funga zao vizuri na kwa utulivu hususani katika kipindi
hiki kigumu cha janga la Ugonjwa wa CORONA " Amesema Sidina.
“Mkurugenzi amenituma niwaambie Waislamu wote kwamba , hiki ni kipindi kizuri kwahiyo wakitumie vizuri na mambo makubwa na faida wataziona maana ni moja ya nguzo za imani katika Uislamu lakini nafasi hii ya mfungo ni muhimu ili kupata Afya njema na swawabu nyingi kutoa kwa Mwenyezi Mungu.””Ameongeza Sidina.
Amesema kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya
Morogoro amewataka Waislamu kukitumia
kipindi hiki kifupi kama njia ya kuomba toba kwa Mola na kuomba mazuri yote
na kuombea wagonjwa, familia , Viongozi Wa Kitaifa ili wafanikishe Yale
wanayotaka kulipeleka Taifa hili mbele zaidi kufikia uchumi Wa kati pamoja na
kuliombea Taifa dhidi ya Janga la CORONA.
Mwisho,
amewataka walezi wa Makao ya Watoto wasiwaachie wakazurura hovyo, kikubwa
wawalinde na wasiende katika sehemu zenye mikusanyiko katika kujikinga na
Ugonjwa wa CORONA.
Naye
Matroni wa Makao hayo, Bi. Khadija Allya, , amemshuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa kuwa karibu sana na Wananchi
wake jambo ambalo linatia matumaini.
“’Tunampongeza
sana huyu mama , kwanza ni mchapakazi lakini sio msaada wa kwanza kutupatia
alishawahi kutukabidhi ndoo za maji , beseni na sabauni kwa ajili ya kujikinga
na CORONA hii imeonesha ni jinsi gani amekuwa karibu na wananchi wake hatuan
cha kumlipa kikubwa tunamuombea dua Mwenyezi Mungu alinde na kumbariki na
kumuongezea zaidi ya kile alichokitoa, hatuishii kwa shukrani tu bali
tutamuandikia barua rasmi ya kumshukuru kwa msaada wake wa kutusadia katika
kupata futari kwa watoto wetu “ Amesema Khadija.
Pia
alienda mbali zaidi kwa kuwaombea dua
kwa Mwenyezi Mungu Viongozi wote wa Mkoa
wa Morogoro akiwemo Mkuu wa Mkoa, Mhe. Loata Sanare, Mkuu wa Wilaya Mhe. Regina
Chonjo, Mkurugenzi wa Manispaa , Sheilla Lukuba na Viongozi wengine kwa kushirikiana vyema
katika kupambana na janga la Ugonjwa wa CORONA .
Post a Comment