Meya Manispaa Morogoro aanza ziara ya kikazi na Choo cha Mtoto wa Kike.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga (kulia) akipokea maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Tubuyu, John Mniko (kushoto) ya ujenzi wa Choo cha mtoto wa kike. |
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga akitoa maelekezo mara baada ya kukagua choo hicho. |
Choo cha Mtoto wa kike kinavyoonekana kwa mbele (kulia ni mlango wa kuuingilia wa kuchangia na kushoto ni mlango wa kuingilia kwa watu wenye ulemavu. |
Mkuu wa Shule ya Sekondari Tubuyu, John Kamunu Mniko akitoa malekezo ya ujenzi wa choo cha mtoto wa kike kwa Mstahiki Meya. |
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, ameanza ziara zake za kikazi za kukagua miradi ya maendeleo katika Manispaa
ya Morogoro ambapo ameanza kutembelea ujenzi wa Choo cha mfano cha mtoto wakike
kilichojengwa Shule ya Sekondari Tubuyu Kata ya Tungi.
Ziara hiyo ameianza leo Mei 15, 2020 kwa kutembelea mradi wa
ujenzi wa Choo cha Mtoto wa kike pamoja na Stendi ya Mabasi Msamvu kwa ajili ya
kuangalia hali ya ukusanyaji wa mapato.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Kihanga, amempongeza
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, kwa usimamizi mzuri na
maono ya kipekee ya kutekeleza kwa haraka na wepesi maagizo ambayo yaliadhimiwa
na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutaka vyoo hivyo vijengwe.
Aidha , amesema kuwa uwepo wa choo cha maalum cha mtoto wa kike
kitamwezesha kukaa shuleni kwa muda mrefu kushiriki masomo kikamilifu badala ya
kubaki nyumbani wakati wa hedhi hali inayoathiri mtiririko wa maudhurio
darasani.
“"Wanafunzi wa kike
wanakabiriwa na changamoto mbalimbali , lakini kama mnavyofahamu tatizo la vyoo katika shule zetu ni kubwa sana
kwani watoto ni wengi na matundu ya vyoo ni machache, nampongeza sana
Mkurugenzi kwa kuliona hili, lakini pia nampongeza na Mkuu wa Shule kwa
usimamizi mzuri bila kuwasahau wahandisi wetu wa Manispaa kwa kutujengea choo
cha mfano ndani ya Mnaispaa yetu na Mkoa kwa ujumla, hivyo nitoe wito kwa wadau
wengine waliopo ndani ya Manispaa yetu kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili
watoto wetu wajisitiri katika vyoo safi na salama ambavyo vitakuwa rafiki kwa
watoto wa kike Shuleni ” Amesema Kihanga.
“ Tunatakiwa kukitunza
hiki ni choo cha mfano, hatujajua wenzetu wamejenga vyoo vya aina gani lakini nina
uhakika tukipata wageni tutawaleta hapa kuja kujifunza, sitarajii tunawaleta
wageni harafu choo mmeshaanza kukiharibu, kitunzeni vizuri hiki ni choo cha
mfano, nitawaleta Waheshimiwa Madiwani kutembelea na kuona kitu
kinachofanyika hapa “ Ameongeza Kihanga.
Kihanga
amesema kutokana na tafiti zilizofanyika kuhusu sababu zinazochangia mahudhurio
hafifu ya mtoto wa kike darasani ni kutokana na mabadiliko ya maumbile
wanapoingia ambapo kuna mifumo ya vyoo visivyofaa kwa matumizi hasa kwa
wasichana wanaoingia hedhi huleta changamoto kubwa kwao.
Hata
hivyo ,amesema Shule za Sekondari zipo nyingi sana na hawana fedha za kutosha lakini
amemuomba Mkurugenzi katika awamu ijayo katika bajeti ya 2021/2022 waweze
kutenga fedha ili waongeze angalau vyoo vyengine ili wasiwe na matabaka tofauti
tofauti .
Katika
hatua nyengine, amewataka waalimu kuendelea kutoa elimu bora kwani mazingira
mazuri ya shule yanaendana na matokeo mazuri.
Amesema
sifa ya Mwalimu ni kufaulisha vizuri , hivyohivyo kwa wazazi pia ni kuona
watoto wao wamefaulu.
Amemtaka
Mkuu wa Shule kusimamia kikamilifu choo hicho mara baada ya kukabidhiwa kwani
imekuwa ni desturi kwa jamii nyingi kitu kinavyoanza kuwa kipya baada ya miezi
miwili uharibifu unafanyika.
Wakati
huo huo amesema ubora wa vyoo vya watoto wa kike uendane na vyoo vya wanaume
ili kuepeuka kutengeneza Taifa lenye matabaka mawili.
Amesema choo hicho mara
baada ya kukamilika kitakuwa na matundu maalumu kwa ajili kuwafikia watoto wa
kike wenye ulemavu.
Naye Mkuu wa Shule ya
Sekondari Tubuyu, John Kamunu Mniko, amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya
Morogoro kwa kujali wanafunzi wa kike kwa kuwajengea choo cha mfano cha mototo wa
kike.
“ Tunampongeza Mkurugenzi
wetu wa Manispaa kwa kweli ametupa heshima sana, tunatambua katika Manispaa yetu
shule zipo nyingi lakini choo hiki kimekuja kujengwa kwetu, tunashukuru ushirikianao
tunaoupata kutoka kwa Afisa elimu wetu, wahandisi wa Manispaa, na Meya kama
hivi umekuja tumefarijika sana tukuhakikishie tu mara baada ya ujenzi huu
kukamilika tunaenda kuongeza angalau ujenzi wa matundu vyoo vya walimu kwakuwa tumejipanga na
haya maligahafi yatakayobakia katika ujenzi huu tutayatumia,” Amesema Mwl
Mniko.
Choo hicho kimejengwa kwa
thamani ya Shilingi Milioni 35 ambapo kinajumuisha matundu 12, matundu 2 ya
walemavu, bafu na sehemu ya kuvalia nguo na kujiangalia baada ya kumaliza haja
zao.
Post a Comment