Header Ads

DC CHONJO AZINDUA UGAWAJI WA VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WADOGO.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, akimkabidhi Kitambulisho Mwenyekiti wa Machinga Wilaya ya Morogoro, Faustine France.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo,akizungumza na Wajasiriamali wakati wa uzinduzi wa Vitambulisho.(kushoto) Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Ruth John.

Mstahiki Meya Manispaa ya ,Morogoro akitoa neno kwa Wajasiriamali mara baada ya uzinduzi wa Vitambulisho kukamilika.
Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akizungumza na Wajasiriamali wakati wa utambulisho wa viongozi.
Afisa Tarafa Manispaa ya Morogoro, Winfred Kipako akisoma utambulisho wa viongozi na wageni katika uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali.
Kaimu Afisa Biashara Manispaa ya  Morogoro Mariam Ngonyani akisoma taarifa ya Wafanyabiashara wadogo na sifa za wanaostahili kupewa Vitambulisho.


Picha ya Pamoja baada ya kukamilika kwa uzinduzi wa awamu ya pili ya  Vitambulisho vya Wajasiriamali wadogo.
Viongozi wa Wamachinga wakionesha Vitambulisho vyao mara baada ya uzinduzi kukamilika.
 

MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo,  amezindua rasmi zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro .

Zoezi hilo la uzinduzi limefanyika leo Mei 29, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Morogoro na kuhudhuriwa na wajasiriamali wadogo, Watendaji wa Kata, Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa, Mwakilishi toka TRA Mkoa wa Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema watakao stahili kupata Vitambulisho hivyo ni Wajasiriamali wenye mtaji usiozidi milioni 4.

Chonjo, amesema ugawaji wa Vitambulisho hivyo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Aidha, amesisitiza kuwa wafanya biashara hao wanatakiwa kuwa waaminifu na kuvitunza vitambulisho hivyo ili visipotee. 

 "Itakuwa kitu cha ajabu kama utagawa kitambulisho chako na kumpa mtu mwingine afanyie biashara, ikibainika kuwa hujawa mwaminifu basi kitambulisho kitanyang'anywa kwa kuwa utakuwa huna sifa ya kuwa na kitambulisho hicho".Amesema Chonjo.

Hata hivyo, amesisitiza na kuwaomba wafanyabiashara wadogo wachangamkie fursa na kujitokeza kwa wingi kuchukua vitambulisho hivyo.



Ametoa rai huku akiwataka wafanyabiashara hao wadogo kutokutumia vitambulisho hivyo kwenda kinyume na sharia zilizopo ikiwa ni pamojana kufanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

""Hatuwapi vitambulisho hivi kama pambo la nyumbani, tunataka kila  Mjasiriamali avae kitambulisho hicho awapo eneo lake la biashara na asimpe mtu mwingine yeyote ili kuepuka usumbufu kwa watu wa mamlaka ya mapato Tanzania (T.R.A)'" Ameongeza DC Chonjo.


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Mazimbu , Mhe. Pascal,  ametoa rai kwa watendaji wote wa kata Manispaa ya Morogoro  kuweka maslahi ya Taifa mbele badala ya matakwa yao binafsi katika zoezi zima la utambuzi wa wafanyabiashara walio katika sekta isiyo rasmi kwa ajili ya ugawaji wa vitambulisho vilivyotolewa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mheshimia Rais Dkt . John Pombe Magufuli.

 Kihanga,  amesema kuwa watendaji wote wanawajibika kufanya zoezi la utambuzi wa wafanyabiashara wadogo wadogo kwa kuzingatia uadilifu wa hali ya juu ili kutoingia katika dosari ya aina yoyote na kwamba mtendaji yoyote asithubutu kutumia udanganyifu katika zoezi.

"'Zoezi hili linahitaji sana  uangalifu wa hali ya juu ili kuepuka ukwepaji kodi kwa kuwasilisha majina yasiyostahili , niwaombe Watendaji mujiepushe na rushwa kwani zoezi hili si la kisiasa bali kiutendaji na ni agizo kutoka kwa Rais hivyo libebwe kwa uzito wake na heshima ya Rais na kwamba mtendaji yoyote atakayebainika kufanya udanganyifu sheria itachukua mkondo wake" Amesema Kihanga.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewapongeza  wafanya biashara hao kwa kutunukiwa vitambulisho hivyo na kuwasihi kuwa wavitumie vitambulisho hivyo kama maelekezo ya Serikali yanayosema. 

"Vitambulisho hivi haviuzwi isipokuwa gharama ya Shilingi elfu ishirini (20,000) ni kuchangia gharama ya kutengeneza vitambulisho hivyo, Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli anawajali sana wafanya biashara ndio maana ameamua kutoa vitambulisho hivyo ili mfanye kazi kwa uhuru bila kubuguziwa na mtu yeyotena kuwa wafanyabiashara wakubwa hapo baadaye. ". Amesema Lukuba.

Lukuba, katika kona zoezi hilo linafanikiwa ametoa jumla ya Shilingi  120,000/= kwa kuwaliapia Viongozi 6  wa Wamachinga Manispaa ya Morogoro ikiwa ni kuleta motisha na kuwafanya Viongozi hao kuwa mabalozi wazuri kwa wafanyabiashara wenzao.

Katika hatua nyengine, Afisa Elimu kwa mlipa  Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Morogoro, Bw. Mogani Isidoli,  amesema wanaostahili kupata vitambulisho hivyo vilivyotolewa na Mhe. Rais ni wale wasio na namba ya utambulisho ya mlipa kodi ya biashara (TIN) na mauzo ghafi ya biashara zao yasiyozidi shilingi milioni 4 kwa mwaka au mauzo ya wastani wa shilingi  elfu 12 kwa siku.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Wamachinga Wilaya ya Morogoro, Ndg.Faustine France, amesema  wamefurahishwa sana na hatua ya Serikali kwa kuwaona kwa jicho la karibu wafanyabiashara wenye mitaji midogo na kuipongeza sana Serikali ya Awamu ya tano chini ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli.


"Tumefurahishwa sana na hatua hii ya kupata tena fursa ya kukabidhiwa vitambulisho, hakika Rais wetu ameamua kutukwamua sisi watu wa hali ya chini, tutazidi kumuombea na ifikapo uchaguzi Mkuu yeye aende Chato sisi tutaungana naey kama SHIUMA kumchukulia fomu aendelee kuwa Rais maana tunayaona matunda na mafanikio makubwa sana ya kiuchumi katika Taifa letu" Amesema Faustine.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.